“Nuku‘alofa, Tonga,” Liahona, Sept. 2022.
Kanisa Liko Hapa
Nuku‘alofa, Tonga
Hekalu la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Nuku‘alofa limejengwa karibu na shule inayomilikiwa na Kanisa ya Shule ya Upili ya Liahona. Waumini wa Kanisa ni asili mia 63 ya idadi ya watu huko Tonga, mahali ambapo Kanisa lina
-
Waumini 66,400 (kwa makadirio)
-
Vigingi 21, wilaya 2, kata na matawi 173, na misheni 2
-
Vituo vya historia ya familia 21, hekalu 1 linalofanya kazi na 1 liko katika hatua za ujenzi
Sisi Tutaunganishwa Tena
Sonasi Langi (sasa ni marehemu) wa Kolonga, Tongatupu, mara kwa mara alikuwa anakusanyika na wanafamilia ili kuimba nyimbo za dini na kuweka maua kwenye makaburi ya baba yake na dada yake. “Siku moja tutaunganika tena,” yeye alisema. “Nadhani tutaimba nyimbo hizi hizi.”
Zaidi kuhusu Kanisa huko Tonga.
-
Maelezo, takwimu, na historia ya Kanisa huko Tonga.
-
Shikilia fimbo ya chuma, Rais Nelson anawaambia waumini kwenye ibada ndogo huko Tonga mwaka 2019.
-
Baada ya mlipuko wa volkano wa Januari 2022, Urais wa Kwanza ulituma barua ya upendo na matumaini huko Tonga.
-
Kanisa linapeleka misaada kutokana na mlipuko wa volkano na tsunami huko Tonga.
-
Waumini huko Tonga wanapeleka bidhaa kwa visiwa vilivyo nje zaidi.
-
Mwandishi wa habari anasimulia kitu alichojifunza kutoka kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wa Tonga kuhusu jinsi ya kuvumilia hadi mwisho.
Mfalme wa Tonga anamkaribisha Rais Russel M. Nelson na mke wake, Wendy; Mzee Gerrit W. Gong na mke wake, Susan; na wengine walipoitembelea Tonga mnamo 2019.
Picha na Jeffrey D. Allred, Deseret News
Kama wasichana Kanisani kote, msichana huyu huko Tonga anaweka malengo na anafanya kazi ili kuyakamilisha.
Kupigwa lipu huku kunaonyesha jinsi Hekalu la Neiafu Tonga litakavyoonekana wakati litakapokwisha kujengwa.
Nyumbani ni kitovu cha kujifunza injili huko Tonga, kama ilivyo kote liliko Kanisa wakati waumini wanapotii wito wa “njoo, unifuate” (Luka 18:22).
Huko Tonga, burudani kamilifu kifamilia inaweza kwa urahisi kabisa kujumuisha matembezi ya pamoja ufukoni mwa bahari.
Kilimo ni muhimu huko Tonga, na Watakatifu wa Siku za Mwisho wanalima na kuvuna chakula chao.
Huko Tonga, kama ilivyo katika jamii za visiwa vingi vya Pasifiki, majani ya migomba ya ndizi mara nyingi yametumika katika maandalizi ya milo ya familia.
Kuimba nyimbo ni sehemu muhimu ya kuabudu pamoja huko Tonga, kama ilivyo kote liliko Kanisa.
Vazi la kitamaduni lina nafasi muhimu katika jamii ya Watonga.
Mvulana anafurahia kukutana na wenzake kwenye shughuli ya vijana kwenye jengo la mikutano huko Tonga.
Kujifunza maandiko kila siku kunawasaidia wanandoa huko Tonga kukua pamoja kiroho.
Mnamo Januari 2022, mlipuko wa volkano ulifunika sehemu nyingi za Tonga kwa majivu.
Picha kutoka Malau Media, imetumika kwa ruhusa
Waumini kwenye kisiwa cha Tongatapu walitoa vitu kama msaada, vilivyobebwa kwa boti ili kuwasaidia wale walio kwenye visiwa vingine vya nje.