2023
Fikiria Selestia!
Novemba 2023


Kikao cha Jumapili Mchana

Fikiria Selestia!

Dondoo

Picha
hekalu

Pakua PDF

Nimejifunza kwamba mpango wa Baba wa Mbinguni kwetu ni wa kupendeza zaidi, kwamba tunachokifanya kwenye maisha haya kina umuhimu sana, na kwamba Upatanisho wa Mwokozi ndio unaoufanya mpango wa Baba kuwezekana. …

… Leo, ili kuwasaidia kustahili baraka tele ambazo Baba wa Mbinguni anazo kwa ajili yenu, ninawalika kuasili utamaduni wa “kufikiria selestia”! …

Hivyo basi, wapendwa akina kaka na dada zangu, ni kwa jinsi gani na wapi na nani ambaye unataka kuishi naye milele? Mnatakiwa kufanya uchaguzi.

Wakati mnapofanya chaguzi, ninawaalika kuwa na mtazamo wa kina—mtazamo wa umilele. Mwekeni Yesu Kristo kwanza, kwa sababu maisha yenu ya milele yanategemea imani yenu Kwake na Upatanisho Wake. Maisha yenu pia yanategemea juu ya utiifu wenu wa sheria Zake. …

Wakati unapofokasi kwenye kufikiria selestia, tazamia kukutana na upinzani. …

Unapofikiria selestia, moyo wako taratibu utabadilika. Utataka kusali zaidi na kwa dhati. …

Unapofikiria selestia, utajikuta ukiepuka chochote ambacho kinakunyang’anya haki yako ya kujiamulia. …

Kufikiria selestia pia kutawasaidia kutii amri ya usafi wa kimwili. …

Mnapofikiria selestia, utayatazama majaribu na upinzani katika njia mpya. …

Wakati mnapofikiria selestia, imani yako itaongezeka. …

Kulipa zaka inahitaji imani, na pia hujenga imani katika Mungu na Mwanawe Mpendwa.

Kuchagua kuishi maisha masafi katika ulimwengu unaochochea ngono, uliojaa siasa hujenga imani.

Kutumia muda zaidi hekaluni hujenga imani.