2023
Kwenye Njia ya Jukumu Lao
Novemba 2023


Kwenye Njia ya Jukumu Lao

Dondoo

Picha
alt text

Pakua PDF

Nina shukrani kwa mamilioni ya waumini wa Kanisa ambao hivi leo huja kwa Mwokozi na kusonga mbele kwenye njia ya agano. … Imani yenu thabiti katika Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo na maisha yenu yasiyo ya kuigiza, yaliyowekwa wakfu hunivutia niwe mtu na mfuasi mwema zaidi.

Ninawapenda. Ninawatamania. Ninawashukuru. Na ninawapongeza.

Kauli moja katika Kitabu cha Mormoni iliyotolewa na Samweli Mlamani inafupisha hisia zangu kwenu vyema zaidi.

“Tazama kwamba sehemu yao kubwa iko katika njia ya jukumu lao … na wanajaribu kwa bidii bila kuchoka ili walete ndugu zao waliosalia kwenye elimu ya ukweli” [Helamani 15:5–6; msisitizo umeongezwa]. …

Mnapenda na mnatumikia, mnasikiliza na kujifunza, kujali na kufariji, na kufundisha na kushuhudia kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Mnafunga na kuomba mara kwa mara, mnaimarika na kuwa imara katika unyenyekevu, na mnakuwa imara zaidi na zaidi katika imani juu ya Kristo, “hadi nafsi [zenu] zikajazwa na shangwe na faraja, ndiyo, hata kwenye kusafishwa na utakaso wa mioyo [yenu], utakaso ambao huja kwa sababu ya … kumtolea Mungu mioyo [yenu]” [Helamani 3:35].

… Ninyi ambao hivi leo mnasonga mbele katika njia ya jukumu lenu ni nguvu ya Kanisa la Mwokozi lililorejeshwa. Na kama Bwana alivyoahidi, “enzi zote na tawala, himaya na nguvu, zitafunuliwa na kuwekwa juu ya wote ambao wamestahimili kwa ujasiri mkubwa kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo” [Mafundisho na Maagano 121:29].