2023
Nguvu ya Kuunganisha
Novemba 2023


Nguvu ya Kuunganisha

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Huwa tunadhani kwamba mamlaka ya kuunganisha yanatumika tu kwa aina fulani ya ibada za hekaluni, lakini mamlaka hayo ni muhimu katika kufanya ibada yoyote kuwa halali na yenye kuunganisha baada ya kifo. …

Uhalali ambao nguvu ya kuunganisha inautoa kwa ibada za ukuhani inajumuisha, ndiyo, ibada zinazofanywa katika mahali ambapo Bwana amepateua—hekalu Lake. … Nguvu hii ya kuunganisha ni dhihirisho kamilifu la haki, rehema na upendo wa Mungu.

Kwa kuweza kuifikia nguvu ya kuunganisha, mioyo yetu kwa kawaida inawageukia wale waliotutangulia. Kusanyiko la siku za mwisho ndani ya agano linavuka ng’ambo ya pazia. …

Dhihirisho la juu zaidi na takatifu zaidi la nguvu ya kuunganisha ni katika unganiko la milele la mwanamume na mwanamke katika ndoa na unganiko la mwanadamu kwa vizazi vyao vyote. …

Tunaweza kuona kwa nini “ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imeamriwa na Mungu na kwamba familia ni kiini cha mpango wa Muumbaji kwa hatma ya milele ya watoto Wake” [“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Maktaba ya Injili]. Wakati huo huo, tunatambua kwamba katika wakati huu usio mkamilifu, huu sio uhalisia au hata uwezekano wa uhalisia kwa baadhi. Lakini tunalo tumaini katika Kristo. …

Ninashuhudia kwamba nguvu na mamlaka ya kuunganisha yaliyorejeshwa duniani kupitia Joseph Smith ni halisi, kwamba kile kilichofungwa duniani ni kweli kimefungwa mbinguni.