2023
Sifa kwa Aliyenena na Bwana
Novemba 2023


Sifa kwa Aliyenena na Bwana

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Wapendwa akina kaka na dada zangu, ushuhuda wangu kwenu asubuhi hii ni kuhusu jinsi ambavyo tumebarikiwa kwa wingi kujua vyote tujuavyo kwa sababu ya Joseph Smith, nabii wa kipindi hiki cha mwisho cha utimilifu wa nyakati.

Tunao uelewa wa dhumuni la maisha, uelewa wa sisi ni nani.

Tunajua Mungu ni nani; tunajua Mwokozi ni nani, kwa sababu tunaye Joseph, ambaye alikwenda kwenye kijisitu kama mvulana, akitafuta msamaha wa dhambi zake.

Nadhani ni moja ya vitu vitukufu na vizuri ambavyo mtu yeyote ulimwenguni anaweza kujua—kwamba Baba yetu wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo Wamejionesha Wenyewe katika siku hizi za mwisho na kwamba Joseph alikuzwa ili kurejesha utimilifu wa injili isiyo na mwisho ya Yesu Kristo.

Tuna kitabu cha Mormoni. Kitabu cha Mormoni ni zawadi ya kupendeza na ya kustaajabisha kiasi gani kwa uumini wa Kanisa. Ni ushahidi mwingine, ushuhuda mwingine kwamba Yesu ndiye Kristo. Tunacho kwa sababu Joseph alikuwa mstahiki wa kwenda na kuchukua mabamba, alipata msukumo wa kimbingu kuyatafsiri kwa kipawa na nguvu za Mungu na kukileta kitabu ulimwenguni. …

… Tuko kwenye mchakato wa kujaribu kujiandaa, siku hadi siku, kuwa bora zaidi, wakarimu zaidi, waliojiandaa zaidi kwa ajili ya siku ile, ambayo kwa hakika itakuja, ambapo tutapita kwenye uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo.