2023
Mpotevu na Njia Ambayo Inaongoza Nyumbani
Novemba 2023


Mpotevu na Njia Ambayo Inaongoza Nyumbani

Dondoo

Picha
alt text

Pakua PDF

Kurejea kwa Mwana Mpotevu, na Richard Burde.

Ni nani miongoni mwetu ambaye hajachepuka kutoka kwenye njia ya utakatifu, kwa upumbavu tukifikiria tungepata furaha zaidi kwa kufuata njia yetu wenyewe?

Ni nani miongoni mwetu ambaye hajahisi kunyenyekezwa, kuvunjika moyo na kutamani sana msamaha na rehema?

Pengine baadhi wanaweza kujiuliza, “Je, inawezekana kurejea? Nitakashifiwa milele, kukataliwa na kuepukwa na rafiki zangu wa zamani? Je, ni bora tu kubaki nimepotea? Je, Mungu atahisi vipi kama nikijaribu kurudi?”

[Lile] fumbo [la Mwana Mpotevu] hutupatia jibu.

Baba yetu wa Mbinguni atatukimbilia sisi, moyo Wake ukifurikwa na upendo na huruma. …

Mbingu zitafurahia kurudi kwetu. …

Ingawa chaguzi zinaweza kukupeleka mbali kutoka kwa Mwokozi na Kanisa Lake, Bwana Mponyaji anasimama kwenye njia iongozayo nyumbani, kukukaribisha wewe. Na sisi kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo tunataka kufuata mfano Wake na kuwakumbatia ninyi kama akina kaka na akina dada zetu, kama marafiki zetu. Tunafurahia na kusherehekea pamoja nanyi. …

Sijifanyi kwamba kurudi ni kitu rahisi kufanya. Ninaweza kushuhudia juu ya hilo. Inaweza, kwa kweli, kuwa uchaguzi mgumu sana ambao utawahi kuufanya.

Lakini ninatoa ushahidi kwamba dakika ile unapoamua kurudi na kutembea katika njia ya Mwokozi na Mkombozi wetu, nguvu Zake zitaingia ndani ya maisha yako na kuyabadilisha.