2023
Kutembea katika Uhusiano wa Agano na Kristo
Novemba 2023


Kutembea katika Uhusiano wa Agano na Kristo

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Bwana atatujibu kila mmoja wetu katika siku yetu ya dhiki ikiwa tutachagua kuunganisha maisha yetu na Yake. Yeye ameahidi kutembea pamoja nasi njiani.

Tunaweza kuita matembezi haya njia ya agano—njia inayoanza na agano la ubatizo na kuongoza kwenye maagano ya kina zaidi tunayoyafanya hekaluni. … Agano si tu kuhusu mkataba, japokuwa hilo ni muhimu. Ni kuhusu uhusiano. …

Yake ni misheni ya upendo. Yesu Kristo atakutana nasi pale tulipo na jinsi tulivyo. Hii ndiyo kwa nini ya bustani, msalaba na kaburi. Mwokozi alitumwa atusaidie tushinde. Lakini kubaki pale tulipo hakutaleta ukombozi tunaoutafuta. … Yake pia ni misheni ya kuinua. Atafanya kazi ndani yetu ili kutuinua mpaka pale Yeye alipo na, kwenye mchakato, anatuwezesha tuwe jinsi Yeye alivyo. Yesu Kristo alikuja kutuinua. Yeye anataka kutusaidia tuwe. Hii ndiyo kwa nini ya hekalu. Lazima tukumbuke: si njia pekee itakayotuinua, ni mwenza—Mwokozi wetu. Na hii ndiyo kwa nini ya uhusiano wa agano. …

… Anzia pale ulipo. Usiruhusu hali yako ikuzuie. Kumbuka, kasi au kujiweka kwenye njia si muhimu kama kupiga hatua. …

Ninashukuru, tunatembea njia hii pamoja, tukiomba kutiwa moyo njiani. Tunaposhiriki uzoefu wetu binafsi pamoja na Kristo tutaimarisha msimamo binafsi.