Liahona
Mtu Mkuu katika Kitabu cha Mormoni
Januari 2024


“Mtu Mkuu katika Kitabu cha Mormoni,” Liahona, Jan. 2024.

Karibu kwenye Toleo Hili

Mtu Mkuu katika Kitabu cha Mormoni

Miaka mingi iliyopita, akina kaka wahudumiaji walinialika kwa bidii kujifunza Kitabu cha Mormoni. Wakati wananipa mwaliko huu, niligundua kwamba, ingawa nilisoma kidogo kutoka Kitabu cha Mormoni kila siku, sikuwa najifunza kukihusu kwa bidii.

Walishiriki nami ahadi ambayo ilitokana na maneno kutoka kwa Rais Ezra Taft Benson: “Kuna nguvu katika hiki [kitabu cha Mormoni] ambayo itaanza kutiririka katika maisha yako wakati utakapoanza kujifunza kitabu hiki kwa bidii. Utapata nguvu kubwa ya kupinga majaribu …kuepuka kudanganywa … kubaki katika njia nyembamba iliyosonga” (Teachings of Presidents of the Church: Ezra Taft Benson [2014], 141).

Nilikubali mwaliko wao, na katika miezi iliyofuatia niliona kwamba ahadi yao ilitimia. Kimebadilisha maisha yangu.

Sababu kuu ambayo Kitabu cha Mormoni kinatoa nguvu za kiroho ni kwamba kinatusogeza sisi karibu zaidi na Yesu Kristo. Katika makala ya Rais Henry B. Eyring kwenye ukurasa wa 4, anaandika, “Wale ambao kwa dhati wanasoma Kitabu cha Mormoni, wanaishi kanuni zake na kusali kuhusu ukweli wake watamhisi Roho Mtakatifu na kuongezeka imani yao katika, na ushuhuda wao juu ya Mwokozi.”

Yesu Kristo ndiye mtu mkuu katika Kitabu cha Mormoni. Kama mwandishi mwenzangu, Madison Sinclair, pamoja nami tunavyoshiriki makala yetu ya, “Jesus Christ in the Book of Mormon” (ukurasa wa 10), kuna zaidi ya marejeleo 7,000 ya Mwokozi katika Kitabu cha Mormoni.

Ninajua kwamba kadiri tunavyojifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu pamoja na Njoo, Unifuate, tutasogea karibu zaidi na Yesu Kristo.

Kwa upendo,

John Hilton III

Profesa wa Elimu ya Dini, Chuo Kikuu cha Brigham Young

Picha
mwanamke akisoma maandiko

Kielelezo na J. Kirk Richards