Liahona
Masafa Sahihi
Januari 2024


“Masafa Sahihi,” Liahona, Jan. 2024.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Masafa Sahihi

Sikuwa nimeelewa kwa nini rubani aliyepotea hakuwasiliana na sisi.

Picha
ndege ndogo ndogo na mnara wa kudhibiti ukiwa nyuma yao

Kielelezo na Roger Motzkusart

Jioni moja wakati wa mafunzo kazini kama mdhibiti wa trafiki ya anga uwanja wa ndege wa Tijuana, Mexico, mimi pamoja na mwelekezaji wangu tuligundua kwamba ukungu mkubwa kutoka baharini umefunika uwanja wote wa ndege na sehemu kubwa ya jiji. Uonekano, hata hivyo, ulikuwa ndani ya mipaka iliyoruhusu ndege kutua na kuondoka.

Punde, tukaona ndege aina ya Cessna 172 inakuja kutoka upande wa kusini kando ya ufukwe, ikiruka kupitia visual flight rules (VFR). Chini ya VFR rubani hutafuta wenyewe kwa kuona kwa pointi za marejeleo ardhini ili kufika wanakoenda.

Kwa bahati mbaya, rubani alipotea katika ukungu. Akiruka kwa kuzunguka ufukweni, alijaribu kujitafutia mwenyewe alama za uwanja, lakini uoni hafifu ulizuia uonaji wake. Nilimwuliza mwelekezaji wangu tungeweza kufanya nini ili kumsaidia.

“Alihitaji kusikika kwenye masafa ya bendi ya mnara wa kudhibiti na kuwasiliana na sisi,” alijibu. “Vinginevyo, hatuwezi kufanya chochote kwa ajili yake.”

Sikuelewa kwa nini rubani yule aliyepotea hakuwasiliana na sisi. “Je, alikuwa na tatizo na redio yake? Je, alifikiri kwamba angeweza kuondokana na hatari yeye mwenyewe?

Dakika zilipita. Mwishowe rubani alisikika kwenye masafa ya mnara ule. Kwa sauti ya hofu, aliomba msaada. Mara moja tukampa maelekezo kumwongoza kwa usalama kwenye njia ya kutua ndege. Alipaswa tu kuamini maelekezo yetu na vyombo vyake vya kurukia.

Kuona ndege ikionekana kutoka kwenye ukungu dakika chache baadaye na kisha akatua kwa usalama kulitupa sisi shangwe isiyoelezeka.

Njiani kurudi nyumbani, nilitafakari kile yule rubani alichopitia. Akituita sisi kwenye bendi sahihi ya anga kulileta tofauti kati ya kupokea msaada au kuruka kwa kuzungukazunguka—au mbaya zaidi.

Kama rubani huyu, ninapotea nyakati zingine katika “ukungu wa giza” (1 Nefi 8:23). Ninapohitaji mwongozo wa Mungu, kwa subira Yeye anasikiliza sauti yangu.

Kama vile tu nilivyoweza kuona ndege iliyopotea katika rada, Baba yetu wa Mbinguni anatuona sisi na changamoto zetu. Ninashukuru kuwa Yeye anatupatia mwongozo. Anatupatia msaada kupitia sala, maandiko, manabii walio hai na kipawa cha Roho Mtakatifu. Yeye atatuongoza sisi kutoka hatari za kimwili na kiroho kama tutasikika katika masafa sahihi, tukiomba mwongozo na kusikiliza sauti Yake.