Liahona
Je, Mimi Ninamgeukia Bwana Kwanza?
Januari 2024


“Je, Mimi Ninamgeukia Bwana Kwanza?,” Liahona, Jan. 2024.

Njoo, Unifuate

1 Nefi 11–15

Je, Mimi Ninamgeukia Bwana Kwanza?

Picha
Nefi akisali

Tunajua kutoka 1 Nefi 2:16 kwamba wakati Nefi alipokabiliwa na sintofahamu, yeye alimgeukia Bwana na Bwana alilainisha moyo wake. Kwa upande mwingine, wakati Lamani na Lemueli walipokabiliwa na sintofahamu, walibishana wao kwa wao na kumtegemea ndugu yao Nefi kwa ajili ya majibu badala ya kumtegemea Bwana (ona 1 Nefi 15:8–9).

Lamani na Lemueli walionyesha mtindo wa kile kinachoweza kutokea pale tunapotegemea kila kitu kwa wengine badala ya kumgeukia Mungu. Nefi akawa imara kiroho na kubakia mwaminifu kwa Mungu maisha yake yote, wakati Lamani na Lemueli hatimaye waliachana na mafundisho ya baba yao juu ya Bwana. Ingawa Nefi alikuwa mfuasi wa kuaminika, hata yeye alijua kwamba hakuwa mbadala wa kutafuta ukweli moja kwa moja kutoka kwa Bwana (ona 1 Nefi 15:6–11).

Unapotathmini utegemezi wako kwa Bwana dhidi ya watu wengine, je ni chaguzi ipi kati ya hizi wewe unahusiana nayo?

Vyanzo vya Kiulimwengu

Vyanzo vya Kiinjili

Mara kwa mara nasahau kutafakari na kuangazia juu ya kile nilichofundishwa wakati wa mkutano mkuu.

Siku zote ninajifunza mahubiri ya mkutano mkuu ili kuyaweka maneno ya viongozi kuwa mapya akilini mwangu.

Ninapokuwa na maswali ninaangalia mitandao ya kijamii au podkasti niipendayo ili kupata majibu.

Ninapokuwa na maswali, ninapekua maandiko ili kupata msaada au maneno ya manabii wa kisasa.

Mara nyingi ninasahau kusali na kujifunza maandiko.

Sala na kujifunza maandiko ni sehemu ya kawaida katika maisha yangu.

Watu wengine wana ushauri ulio bora kuliko viongozi wa Kanisa au maandiko.

Ninapata amani katika maneno ya viongozi wa Kanisa na maandiko.

Ninathamini maoni ya watu wengine zaidi kuliko mafundisho ya injili.

Ninathamini mafundisho ya injili na miongozo ya kiungu kutoka kwaa Roho Mtakatifu.