Liahona
Kwa Nini Mungu Alikuwa Habadilishi Maisha Yangu?Hakubadilisha Maisha Yangu?
Januari 2024


“Kwa Nini Mungu Alikuwa Habadilishi Maisha Yangu?Hakubadilisha Maisha Yangu?,” Liahona, Jan. 2024.

Vijana Wakubwa

Kwa Nini Mungu Alikuwa Habadilishi Maisha Yangu?Hakubadilisha Maisha Yangu?

Ndoa yangu ilipogeuka kuwa jinamizi, nilijifunza kuhusu nguvu ya haki ya kujiamulia.

Picha
mkono umeshika kalamu na kuandika katika kitabu kilicho wazi

Nilipokuwa na umri wa miaka 23 niliunganishwa hekaluni kwa mwanaume wa ndoto zangu. Siwezi kukumbuka siku yoyote ya furaha katika maisha yangu yote kama siku hiyo.

Lakini kila kitu ambacho daima nilikitegemea kwa ajili ya maisha yangu kilianza kuporomoka kwa kasi ya haraka sana. Mume wangu alikua akiongezeka kimwili na kihisia kiunyanyasaji kwangu mimi.

Nilihisi mwenye kuchanganyikiwa na mwenye maumivu. Sikuwa naelewa kwa nini uaminifu wangu haukuwa ukionekana kufanya tofauti katika ndoa yangu. Nimehudumu misheni, nilishika maagano, nilifuata amri na hata kuhudumu kama mfanyakazi wa hekaluni. Lakini bila kujali kiasi gani nilijaribu kukua na kuwa karibu zaidi na Yesu Kristo, ndoa yangu iliendelea kuwa ngumu zaidi.

Nikiangalia nyuma, nilitambua kwamba hata ingawa kwa sala nilifikiria kama ningefunga ndoa na mume wangu na kuwa na imani kwamba tungeweza kufanyia kazi kuyatatua matatizo yetu, nilipuuzia ishara za matatizo yamkini ambayo baadaye yaliibuka katika ndoa yetu.

Kupata Majibu

Baada ya miaka mitano ya upweke na unyanyasaji, uhusiano wangu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ulikuwa ukitetereka. Matarajio yangu kwa ajili ya maisha yangu yaliporomoka na kutofikika.

Nilihisi nimevunjika.

Ilipoonekana dhahiri kwamba mume wangu hakuwa tayari kubadilika, nilianza kumwomba Baba wa Mbinguni anikomboe kutokana na hali yangu au anionyeshe njia sahihi ya mimi kuchukua. Lakini majibu niliyohitaji yalipokuwa hayaji, nilianza kumlaumu Baba wa Mbinguni kama sababu ya maumivu yangu.

Niliendelea kuhudhuria kanisani na kushika maagano yangu, lakini moyo wangu ulikuwa umejaa chuki kwa kukosa mwelekeo.

Kisha siku moja nikatambua kwamba mimi nilikuwa na jibu la hali yangu—nilipaswa kutumia haki yangu ya kujiamulia kutenda na kubadilisha hali zangu. Na nilijua ni uamuzi gani ungekuwa bora kwangu kuuchukua nikiwa na lengo langu la mwisho la kurudi kwa Baba yangu wa Mbinguni.

Mwishowe niliamua kuchukua hatua moja kusonga mbele: Niliongea na mume wangu, na kimuujiza, tulimaliza uhusiano wetu kwa maelewano.

Nguvu ya Kuchagua

Uzoefu huu mgumu ulinisaidia kujifunza kuhusu nguvu na umuhimu mkubwa wa zawaidi tuliyopewa na Mungu ya haki ya kujiamulia.

Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, amefundisha: “Tukiangalia nyuma, tunaweza kuona ni tofauti kubwa kiasi gani ambayo baadhi ya chaguzi zetu tulizofanya katika maisha yetu imeyaleta. Tunafanya maamuzi na chaguzi nzuri ikiwa tutatazama mibadala yake na kutafakari wapi itatuongoza. Tunapofanya hivyo, tutakuwa tukifuata ushauri wa Rais Russell M. Nelson wa kuanza na mwisho akilini. Kwetu sisi, mwisho daima uko kwenye njia ya agano kupitia hekaluni hadi kwenye uzima wa milele, zawadi ambayo ni kuu katika zawadi zote za Mungu.”1

Niligundua kwamba Baba wa Mbinguni hataingilia kati haki ya kujiamulia ya mtu yeyote—Aliniacha mimi nifanye uamuzi wangu mwenyewe wa kufunga ndoa na mume wangu. Yeye pia asingemlazimisha mume wangu kubadilika, hata ingawa mimi nilikuwa ninashikilia maagano yangu, kwa sababu ndoa ya milele inahitaji jitihada zote za kiroho na kimwili kutoka kwa watu wote wawili wanapokuwa wanamfuata Yesu Kristo.

Tunapokabiliwa na mapambano, tunaweza kutumia haki yetu ya kujiamulia kubadilisha mitazamo yetu, na hata sisi wenyewe. Hiyo ndio zawadi ya kiungu ya haki ya kujiamulia. Baba wa Mbinguni anatutaka tumtafute Yeye na Roho na kisha tujiamini sisi wenyewe kufanya maamuzi yaliyo bora zaidi kwa ajili ya maisha yetu.

Mgeukie Mwokozi

Mwanzoni nilitegemea kupona na kuendelea kwa haraka kutokana na ndoa yangu yenye unyanyasaji, lakini mchakato umekuwa wa polepole na mgumu. Kupitia zana za tiba, kusikiliza jumbe za manabii, kusoma maandiko, kusali na kuhisi upendo na msaada kutoka kwa marafiki na familia, ninahisi matumaini ya siku bora za baadaye. Ninapotumia haki yangu ya kujiamulia kutafuta uponyaji, ninatazamia maisha ambayo yanashirikisha msamaha na uhusiano mzuri na wengine, ikijumuisha Mwokozi.

Kwa ongezeko la uelewa wa jinsi gani ya kutumia haki ya kujiamulia katika maisha yangu, uchungu wangu kwa Mungu umegeuka kuwa uelewa, na uhusiano wangu na Yeye umeweza kupona.

Huu ndio uzuri wa injili—kufanya chaguzi zetu wenyewe za kuja kwa Kristo, kufanyia kazi ushauri tupatao kutoka kwa manabii ambao hutuhimiza kutumia haki yetu ya kujiamulia kumtumainia Bwana, na kutengeneza maisha mazuri yaliyojaa imani.

Kama Dada Camille N. Johnson, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi, alivyofundisha: “Kanuni muhimu ya haki ya kujiamulia bila shaka, huturuhusu kuandika hadithi zetu wenyewe. … Lakini Yesu Kristo husimama tayari kututukia kama vyombo vitakatifu … ili kuleta ufanisi … ikiwa [tuna] imani ya kumruhusu Yeye kufanya hilo, kama [tuta] mruhusu kuandika hadithi [yetu] wenyewe.2

Kumaliza ndoa yangu ilikuwa moja ya jambo lililoniuma sana ambalo sijawahi kulikabili. Lakini nimejifunza kwamba unapokabiliwa na jaribu usilolitarajia katika maisha, tunaweza kuomba mwongozo wa kiroho na kufanya maamuzi ambayo yanatusogeza mbele kwenye njia ya agano. Kwa kuwafuata Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, tunaweza daima kuwa na matumaini katika mambo mema na katika baraka Zao walizoahidi za amani na shangwe.

Mwandishi anaishi huko Chile.