Liahona
Kupata Nuru ya Mwokozi katika Kitabu cha Mormoni
Januari 2024


“Kupata Nuru ya Mwokozi katika Kitabu cha Mormoni,” Liahona, Jan. 2024.

Kwa ajili ya Wazazi

Kupata Nuru ya Mwokozi katika Kitabu cha Mormoni

Picha
familia ikisoma pamoja

Wapendwa Wazazi,

Toleo la mwezi huu linatoa utambuzi kuhusu Kitabu cha Mormoni kama mtaala wa Njoo, Unifuate kwa mwaka 2024. Makala zifuatazo hapo chini zinajadili vitu vya msingi kwa ajili ya kupata nuru na kweli katika ulimwengu ambao mara nyingi umejawa na giza na mkanganyiko.

Mijadala ya Injili

Kutafuta Nuru ya Mwokozi

Zingatia kushiriki na familia yako baadhi ya mawazo kutoka katika makala ya Rais Eyring kwenye ukurasa wa 4, na jadili kuhusu jukumu ambalo nuru hiyo inafanya katika maisha yetu. Rejelea hadithi ya Kamryn kuhusu kumtafuta Mwokozi katika giza. Je, ni kwa jinsi gani familia yako inapata nuru ya Mwokozi kupitia kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni mwaka huu?

Wapi Tupekue kwa ajili ya Ukweli

Mungu ndiye chanzo cha ukweli wote, na tunaweza kujifunza ukweli Wake kwa kuutafuta kwa bidii. Mzee na Dada Silva walihitaji kuamua wapi waishi baada ya kurudi kutoka misheni yao, hivyo walitafuta mwangozo kutoka kwa Bwana (ona ukurasa 20). Ni lini Bwana alikupa mwongozo uliouhitaji?

Ona Zaidi katika Kujijifunza Kwako Injili

Wakati wakitembelea jumba la makumbusho ya sanaa, watu mara nyingi wanakimbilia kila kitu wanachoweza kuona, kusababisha wao kuweza kukosa uzuri wa sanaa hiyo. Vile vile, wasomaji wa Kitabu cha Mormoni wanaweza kukosa ukweli muhimu kama waharakisha katika kusoma. Ni mikakati gani inaweza kutusaidia sisi kuchukua uangalifu mkubwa kwenye kitabu hiki cha maandiko? Ona ukurasa 12 kwa ajili ya baadhi ya mawazo.

Njoo, Unifuate Burudani ya Familia

Njia Nyembamba Iliyosonga

1 Nefi 8; 11; 15

Kula tunda la mti wa uzima ni ishara ya kuchagua uzima wa milele kupitia Yesu Kristo (ona 1 Nefi 15:36; Mafundisho na Maagano 14:7). Jaribu shughuli hii ili kujifunza jinsi gani fimbo ya chuma (neno la Mungu) inatuongoza sisi kwenye zawadi hii kuu ya Mungu.

  1. Bandika picha ya mti wa uzima juu ya ukuta.

  2. Bandika uzi (ukiwakilisha fimbo ya chuma) chini ya hiyo picha, na mtu mmoja asimame upande mwingine wa chumba akishika mwisho wa huo uzi.

  3. Weka ni kiasi gani cha muda itachukua kwa mtoto aliyezibwa macho kutembea kutoka mwisho mmoja wa chumba hadi kwenye mti wa uzima bila kushikilia uzi.

  4. Sasa weka ni kiasi gani cha muda kitatumika kufikia mti wa uzima wakati akishikilia uzi ule.

Jadili: Je, tunaweza kufanya nini ili kushikilia kwenye fimbo ya chuma na kamwe tusiiachilie?