2023
Sheria ya Mfungo na Matoleo ya Mfungo
Desemba 2023


Dondoo za Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Sheria ya Mfungo na Matoleo ya Mfungo

Bwana ameweka sheria ya mfungo na matoleo ya mfungo ili kuwabariki watu Wake na kuweka njia kwa ajili ya watoto hao kuwatumikia wenye mahitaji. Sheria ya mfungo huwabariki wote mtoaji na mpokeaji. Waumini husogea karibu na Bwana na kuongezeka katika nguvu za kiroho wanapoishi sheria ya mfungo. Pia huimarisha kujitegemea kwao na kukuza huruma kuu. (Ona Isaya 58:6–12Malaki 3:8–12.)

Kufunga kunaweza kufanywa muda wowote. Hata hivyo, waumini kwa kawaida hufanya Sabato ya kwanza ya mwezi kama siku ya mfungo. Siku ya mfungo kwa kawaida hujumuisha yafuatayo:

  • Kusali

  • Kutokula wala kuywa kwa kipindi cha saa 24 (kama mtu anaweza)

  • Kutoa matoleo ya mfungo

Matoleo ya mfungo ni michango ya kuwasaidia wale wenye mahitaji. Waumini wanapofunga, wanaalikwa kuchangia matoleo ambayo ni sawa na thamani ya milo ambayo hawajaila. Waumini wanahimizwa kuwa wakarimu na kutoa zaidi ya thamani ya milo hii kama wanaweza.

Waumini wanaweza kutoa matoleo yao ya mfungo kupitia fomu ya Zaka na Matoleo Mengine kwa askofu au mmjoa wa washauri wake. Katika baadhi ya maeneo, wanaweza pia kutoa mchango mtandaoni. Katika baadhi ya kata, Askfou anaweza kuwaruhusu wenye Ukuhani wa Haruni wakusanye matoleo ya mfungo (ona 34.3.2).

Chanzo: Kitabu cha Maelezo ya Jumla 22.2.2.