2015
Sifa za Yesu Kristo: Bila Hila ama Unafiki
Aprili 2015


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji

Sifa za Yesu Kristo: Bila Hila ama Unafiki

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kueleza. Je ni kwa namna gani kuelewa maisha na nafasi za Mwokozi kunaweza kuongeza imani yako Kwake na kuwabariki wale unaowaongoza kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

Picha

Kuelewa kwamba Yesu Kristo hana hila wala unafiki kutatusaidia sisi kujitahidi kwa uaminifu kufuata mfano wake. Mzee Joseph B. Wirthlin (1917–2008) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Kulaghai ni kudanganya au kupotosha. Mtu asiye na hila ni mtu asiye na hatia, mwenye dhamira aminifu, na nia safi, ambaye maisha yake yanaonyesha matendo rahisi yanayothibitisha vitendo vyake vya kila siku na kanuni za uadilifu. Naamini umuhimu wa waumini wa Kanisa kuwa bila hila kunaweza kuhitajika zaidi sasa kuliko wakati mwingine kwa sababu wengi katika dunia hii wanaonekana hawaelewi umuhimu wa maadili haya.”1

Juu ya unafiki, Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema: “Hakuna yeyote miongoni mwetu ambaye yu kabisa kama Kristo kama tunavyojua tunapaswa kuwa. Lakini tunatamani kwa dhati kushinda makosa yetu na tamaa ya kutenda dhambi. Kwa moyo na nafsi yetu tunatamani kuwa bora zaidi kwa msaada wa Upatanisho wa Yesu Kristo.”2

“Tunajua tutahukumiwa kulingana na matendo yetu, tamaa za mioyo yetu, na aina ya watu ambao tumekuwa.”3 Hata hivyo tunpojitahidi kutubu, tutakuwa wasafi zaidi—“na heri wenye moyo safi: maana watamwona Mungu” (Mathayo 5:8).

Maandiko ya Ziada

Zaburi 32:2; Yakobo 3:17; 1 Petro 2:1–2, 22

Kutoka katika Maandiko

Watoto wadogo hawana hila. Yesu Kristo alisema: “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Akawakumbatia [watoto] akawaweka mikono yake juu yao, akawabariki” (Marko 10:14, 16).

Kristo pia aliwahudumia watoto katika Amerika baada ya Kusulibiwa Kwake. Aliamuru kwamba watu wawalete watoto wao wadogo Kwake na “kuwaweka chini juu ya ardhi kumzunguka, na Yesu alisimama kati,

[Na] alilia, na umati ulishuhudia hii, na akachukua watoto wao wachanga, mmoja mmoja, na kuwabariki, na kuomba kwa Baba juu yao. …

Na walipotazama kuona walielekeza macho yao mbinguni, na wakaona malaika wakiteremka kutoka mbinguni kama wakiwa katikati ya moto; na walikuja chini na kuzunguka wale wachanga, na malaika waliwahudumia” (3 Nefi 17:12, 21, 24).

Muhtasari

  1. Joseph B. Wirthlin, “Bila Hila,” Ensign, Mei 1988, 80, 81.

  2. Dieter F. Uchtdorf, Njoo, Jiunge Nasi, Liahona, Nov. 2013, 23.

  3. Handbook 2: Administering the Church (2010), 8.1.3.