2015
Ahadi Zake za Wakati Wote
Aprili 2015


Ahadi Zake za Wakati Wote

Robyn Casper, Utah, USA

Picha
drawing of a broken bike

Vielelezo na Bradley H. Clark

Nilipokaa kwenye mkutano wa sakramenti nikitafakari sala ya kubariki mkate, maneno yaliendelea kujirudia yenyewe katika fikra zangu: “kwamba daima Roho wake apate kuwa pamoja nao” (Moroni 4:3; D&C 20:77).

“Daima,” ilisema—siyo kwa wakati fulani tu. Kwanini, wakati huo, miezi kadhaa iliyopita, mume wangu na mimi hatukuweza kuongozwa juu ya kumlinda kijana wetu wa miaka 11 kabla hajauawa kwa ajali ya baiskeli kugongwa na gari? Kwanini Baba wa Mbinguni siyo mara zote anatulinda na kutuonya sisi?

Nilifundishwa katika darasa la watoto na niliamini kwamba Roho Mtakatifu angetulinda. Angetumia sauti ndogo nyembaba kutulinda, kutuongoza, na kututahadharisha na hatari. Mawazo haya yamekuwa katika akili yangu toka Ben alipofariki. Nilimkosa sana, na moyo wangu uliuma kwa kutaka kuelewa na amani.

Sauti yangu ya kuonya ilikuwa wapi? Roho Mtakatifu Alikuwa wapi? Nilihisi kwamba tulikuwa tukifanya vyema kuwa wema. Tulilipa zaka yetu, tulihudhuria mikutano, na kutumikia pale tulipotakiwa kutumikia. Tulikuwa mbali na ukamilifu, lakini tulifanya jioni ya familia na kujifunza maandiko. Tulikuwa tunajaribu.

Muda kama huu nilikuwa nimekaa katika darasa la Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wakati mwalimu alipoelezea historia ya ndugu wa karibu. Wakati akisubiria kwenye mataa, ndugu alihisi msukumo wa kubaki pale aliposimama wakati taa za kijani zilipowaka. Aliusikiliza mwongozo ule, na muda mfupi gari kubwa likaja kukatiza kwenye makutano, likipita kwenye taa nyekundu. Kama asingesikiliza na kutii sauti ile, yeye na watoto wake wangeweza kujeruhiwa au hata kuuawa.

Habari hii ilinigusa sana, lakini nilipokaa katika kiti changu nikilia nikijiandaa kusimama na kuondoka, ufariji mkubwa ulinisafisha. Nilihisi amani kwamba Roho Mtakatifu hakika alikuwa pamoja nami. Kwa upande wangu Hakuwepo pale kama sauti ya tahadhali bali kama mfariji.

Tokea wakati wa ajali ya Ben, nimehisi nguvu kuliko zangu mwenyewe na nimefarijiwa kwa upendo wa Baba yangu wa Mbinguni. Nilikosa uelewa wakati fulani wa kwanini baadhi ya vitu hutokea, lakini sijawahi kuwa na wasiwasi wa upendo Wake.

Nina imani kwamba Mungu anaelewa mambo yote na kamwe hatoniacha bila ufariji. Roho Mtakatifu ana nafasi nyingi katika maisha yetu. Anaweza kutulinda, lakini pia Anatuongoza, anatufariji, anatufundisha, na huleta uelewa na baraka nyingine.

Nilijifunza kwamba Baba wa Mbinguni hutimiza ahadi Zake. Mara zote amekuwa pamoja nami.