2015
Imba Wimbo Wako Unaoupenda
Aprili 2015


Imba Wimbo Wako Unaoupenda

Angela Olsen Center, Ohio, Marekani

Picha
drawing of mother and newborn in hospital

Vielelezo na Bradley H. Clark

Nilikuwa nimejifungua binti yetu, Rebeka. Uchungu wa kujifungua kwangu ulikuwa mkali, na nilikuwa nimechoka.

Wakati Rebeka akiwekwa katika mikono yangu, nilijawa na hisia kwamba nilipaswa niimbe wimbo wangu ninaoupendao, “Mimi Mwana wa Mungu” (Nyimbo, nambari 301). Jibu langu la awali lilikuwa, “Hapana, nimechoka sana. Nitamwimbia baadaye.” Lakini wazo likaja tena. Hivyo, ingawa nilikuwa nimechoka, nilianza kuimba mstari wa kwanza. Mume wangu na mama yangu walijiunga nami.

Tulipomaliza wimbo, nilihisi hisia mzuri katika chumba hicho. Hata daktari, ambaye hadi hatua hiyo alikuwa ametenda kitaaluma zaidi na kuwa katika dunia yake, machozi yalimwagika usoni mwake. Alitushukuru kwa kuimba wimbo mzuri kama huo. Alisema kuwa katika miaka yote yeye akiwa anazalisha watoto, hakuwahi kujisikia kama ilivyokuwa kwa wakati huo.

Niliwazia tukio hilo na kufikiria kama nilipaswa kutafuta rekodi ya wimbo huo na kumpa. Kwa bahati mbaya, nilishughulika sana na maisha na nikasahau juu ya jambo hilo.

Kisha siku ikaja ya kutazamwa kwangu baada ya kujifungua. Daktari alipoingia chumbani, uso wake uking’aa, na kunikumbatia. Alisema hakuweza kuutoa wimbo huo akilini mwake na alikuwa hata amejaribu kupata muziki huo katika mtandao ili aweze kuuimbia familia yake. Hapo ndipo Roho Mtakatifu aliponikumbusha kwamba nilipaswa nipate nakala ya muziki kwa ajili yake. Nilimuahidi kwamba wiki hiyo ningerudi na muziki huo.

Usiku huo niliomba msaada ili kupata mpangilio wa wimbo ambao ungekuwa bora zaidi kwake. Alasiri iliyofuata nilinunua CD iliyokuwa na wimbo huo. Ilipofika katika sanduku la posta siku chache baadaye, sikuweza kungojea kumpa.

Alikuwa na furaha kubwa kuupokea na akanishukuru kwa zawadi. Aliniambia kuwa hakuwa na uhakika ni kwa nini, lakini wimbo huu ulikuwa muhimu sana kwake kushirikiana na familia yake. Tulipoendelea kuzungumza, nilimwelezea si tu upendo wangu wa wimbo huo lakini pia ushuhuda wangu wa ukweli rahisi unaofundisha.

Nilipoendesha gari kwenda nyumbani siku hiyo, nilihisi upendo wa Baba yetu wa Mbinguni kwa mmoja wa binti zake—daktari wangu. Anamjua na kumpenda, na anamtaka aelewe kwamba yeye pia anaweza kurudi kuishi Naye tena.