2015
Umaizi
Aprili 2015


Umaizi

Ninawezaje kuipa kipaumbele jioni ya familia?

“Unapofanya kazi kuimarisha familia yako na kujenga amani, kumbuka jioni ya familia nyumbani kila wiki. Tahadhari usifanye jioni yenu ya familia nyumbani kuwa kitu cha ziada baada ya siku yenye shughuli nyingi. Amua kuwa Jumatatu usiku familia yako itakuwa pamoja nyumbani kwa jioni hiyo. Usikubali mahitaji ya kikazi, michezo, starehe, kazi ya ziada shuleni au kitu kingine chochote kuwa muhimu kuliko muda huo mnaotumia pamoja nyumbani na familia yako.

Muundo wa jioni yenu si muhimu kama muda uliowekezwa mle. Injili inapaswa kufundishwa kwa njia rasmi na kwa njia isiyo rasmi. Fanya iwe tukio lenye maana kwa kila mwanafamilia.”

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “Fanya Matumizi ya Imani kuwa Kipaumbele Chako,” Liahona, Nov. 2014, 94.