2015
Ninajua kuwa Yesu ananipenda
Aprili 2015


Kwa Watoto Wadogo

Ninajua Kwamba Yesu Ananipenda

Mwandishi anaishi katika Colorado, Marekani.

Laney alikuwa anajaribu sana kuwa na staha kanisani. Lakini alikuwa amechoka, miguu yake ilianza kulegea.

Baada ya sakramenti kuisha, Laney alifungua kitabu chake juu ya Yesu. Alipata picha ya Yesu na watoto wadogo. Ilimfanya kusikia amani na furaha ndani yake.

Baada ya mkutano wa sakramenti kumalizika, Laney alimwuliza Mama, “Kwa nini ni rahisi kuwa na staha ninapotazama kitabu changu juu ya Yesu?”

“Ninafikiri ni kwa sababu kinakukumbusha jinsi Yesu anavyokupenda,” Mama akasema.

Laney alikubali kwa kichwa. “Unafikiri Yesu anajua kuwa ninampenda pia?” akauliza.

Mama akamkumbatia Laney. “Ndiyo nina hakika anajua.”