2015
Njia Sahihi
Aprili 2015


Njia Sahihi

Kutoka “Tusipite Kwenye Njia Isiyo sahihi,” Liahona, May 2014, 39–41.

“Yasikilizeni maneno ya yule Mungu aliyewaumba ninyi” (M&M 43:23).

Miaka mingi iliyopita familia yangu na mimi tulitembelea Mbuga ya Taifa ya Arches huko Utah, Marekani. Mojawapo ya matao maarufu katika mbuga ni Delicate arch, na tuliamua kukwea mlima ili kuifikia.

Tulianza kwa hamasa, lakini baada ya muda wengine walitaka kupumzika. Nilikuwa nataka kufika huko haraka kwa hivyo nikaenda pekee yangu. Bila kuwa mwangalifu kwa njia niliyopaswa kuchukua, nilianza kumfuata mtu aliyeonekana kama alifahamu aliko kuwa akienda.

Njia ikawa ngumu zaidi kupanda. Nilikuwa na hakika kwamba familia yangu haingeifikia. Mara nikaona Delicate Arch, lakini kwa mshangao wangu nisingeweza kuifikia Njia niliyofuata haikuelekeza kwenye tao.

Nilivunjika moyo na nikarudi nyuma. Nilingoja kwa wasiwasi hadi nilipokutana na kundi langu tena. Waliniambia kuwa walikuwa wamefuata ishara zilizoonyesha njia sahihi, na kwa uangalifu na bidii walikuwa wamefika Delicate Arch. Kwa bahati mbaya, nilikuwa nimechukua njia isiyo sahihi Ni somo lipi nilijifunza!

Usipotoke kutoka katika njia yako ya kuelekea uzima wa milele na Baba yako wa Mbinguni Fuata kanuni za injili na amri unazojifunza, na utakuwa kwenye njia ya kuishi naye milele.