2015
Huduma ya Mwokozi Isiyo na Ubinafsi na Takatifu
Aprili 2015


Dhabihu ya Mwokozi Isiyo na Ubinafsi

Kutoka katika hotuba ya mkutano wa ibada, “Truths Most Worth Knowing,” delivered kule Chuo Kikuu cha Brigham Young mnamo Nov. 6, 2011. Kwa nakala nzima katika Kingereza, nenda speeches.byu.edu.

Bwana yupo daima. Aliteseka na kulipa deni kama uko tayari kumkubali yeye kama Mkombozi wako.

Picha
Christ in Gethsemane.

Sote tunaishi kwa deni la kiroho. Kwa njia moja au nyingine, akaunti ukua na kukua. Kama unalipa unavyosonga mbele, utakuwa na machache ya kuhofia. Punde unapoanza kujifunza nidhamu na kujua kwamba kuna siku ya kiama mbele. Jifunze kulipa akaunti ya kiroho kwa wakati ufaao badala ya kungojea hadi riba inakusanywa na adhabu.

Kwa sababu mnajaribiwa, mnatarajiwa kufanya makosa fulani. Nadhania kwamba mmefanya mambo maishani mwenu ambayo mnajutia, mambo ambayo hamwezi hata kuomba msamaha hata kurekebisha; kwa hivyo, mnabeba mzigo. Ni wakati wa kutumia neno hatia ambayo inaweza kututia dosari kama wino usioweza kufutika kwa urahisi. Mtoto wa kambo wa hatia ni kuvunjika moyo, kujutia baraka na fursa zilizopotezwa.

Kama unahangaika na hatia, hauna tofauti na watu wa Kitabu cha Mormoni ambao nabii aliwaongelea, “Kwa sababu ya dhambi zao kanisa lilianza kufifia; na wakaanza kutokuamini katika roho wa unabii na roho wa ufunuo; na hukumu za Mungu zikawatazama wao nyusoni” (Helamani 4:23).

Mara nyingi tunajaribu kutatua shida za hatia kwa kumwambia mtu mwengine na kujiambia sisi wenyewe kwamba haidhuru Lakini kwa kiasi fulani, ndani yetu, hatuamini hivyo. Wala hatuamini sisi wenyewe kama tunasema hivyo. Tunajua vyema ni muhimu!

Manabii daima wamefunza toba. Alma alisema, “Tazama, anakuja kukomboa wale watakaobatizwa kutokana na toba, kupitia imani katika jina lake” (Alma 9:27).

Alma alimwambia mwanawe mpotovu wazi wazi, “Sasa, toba haiwezi kuja kwa watu isipokuwa kuwe na adhabu, kama ilivyo pia ya milele kama vile maisha yanapaswa kuwa, ilivyo kinyume na mpango wa furaha” (Alma 42:16).

Kuna madhumuni mawili ya kimsingi kwa maisha ya duniani. Kwanza ni kupokea mwili, ambao unaweza, kama tutapendelea, ukatakaswa na kuinuliwa na kuishi milele. Madhumuni ya pili ni kujaribiwa. Katika majaribio, kwa kweli tutafanya makosa. Lakini kama tutapendelea, tunaweza kujifunza kutokana na makosa yetu. Kama tunasema kwamba sisi hatujatenda dhambi, tunamfanya yeye kuwa mwongo, na neno hatunalo sisi” (1 Yohana 1:10).

Wewe labda unaweza kuhisi upungufu katika akili na mwili na unafadhaika au kulemewa na mzigo wa akaunti ya kiroho ambayo imetiwa alama “wakati umepita.” Unapokumbana ana kwa ana na wewe mwenyewe katika nyakati kama hizo za tafakari za kimya (ambazo wengi wetu wanajaribu kukwepa), kuna mambo ambayo hayajasuluhishwa ambayo yanakusumbua? Una chochote katika dhamiri yako? Bado wewe, kwa kiwango kimoja au kingine, una hatia ya chochote kidogo au kikubwa?

Mara nyingi sana, tunapokea barua kutoka kwa wale ambao wamefanya makosa makubwa au wamelemewa na mzigo. Wanaomba kujua, Je naweza kusamehewa? Naweza kabisa kubadilika? Jibu ni ndio!

Paulo aliwafunza Wakorintho, Hayajaondolewa kwenu majaribu bali kama ilivyo kawaida kwa mwanadamu: Lakini Mungu ni mwaminifu, hatakubali ujaribiwe zaidi ya uwezo wako; bali kwa majaribu pia atafanya njia ya kuponyokea, kwamba uweze kuyastahimili (1 Wakorintho 10:13).

Injili inatufunza kwamba ahueni kutokana na mateso na hatia inaweza kupatikana kupitia toba. Isipokuwa kwa wachache—wale wachache tu—wanaoasi hata jahamamu baada ya kujua utimilifu, hamna tabia, hamna ulevi, hamna uasi, hamna dhambi, hamna kosa, dogo au kubwa, ambalo limesamehewa kutokana na ahadi ya msamaha kamili. Licha ya kilichofanyika katika maisha yako, Bwana ametayarisha njia ya kurudi kama utasikia maongozi ya Roho Mtakatifu.

Wengine wamejawa na mvuto wa nguvu sana, majaribu ambayo hujirudia tena na tena mawazoni mwao, pengine hata kuwa tabia, na kisha ulevi. Tu wadhaifu kwa baadhi ya makosa na dhambi na pia kusema kwamba hatuna hatia kwa sababu tumezaliwa hivyo. Tunaingia katika mtego, na kisha uchungu na mateso yakaja ambayo Mwokozi tu ndiye anayeweza kuponya. Una uwezo wa kuacha na kukombolewa.

Shetani Hushambulia Familia

Rais Marion G. Romney (1897–1988) aliniambia wakati mmoja, “Usiwaambie tu ili waweze kukuelewa; waambie ili kwamba wasiweze kukosa kukuelewa.”

Nefi alisema, “Kwani roho hufurahia uwazi; kwani kwa jinsi hii Bwana Mungu hutenda kazi miongoni mwa watoto wa watu. Kwani Bwana Mungu hutoa nuru hata tupate ufahamu” (2 Nefi 31:3).

Kwa hivyo sikilizeni! Nitaongea wazi wazi kama mtu aliyeitwa na aliye chini ya sharti la kufanya hivyo.

Mnajua kwamba kuna adui. Maandiko yanamwita kwa maneno haya: “Yule nyoka mzee, ambaye ni shetani … baba wa uongo wote.” (2 Nefi 2:18). Alitupwa nje mwanzoni (ona M&M 29:36–38) na kunyimwa mwili wenye kufa. Yeye sasa ameapa kudhoofisha “mpango mkuu wa furaha” (Alma 42:8) na kuwa adui wa wema wote. Yeye analenga mashambulizi yake kwenye familia.

Mnaishi katika siku ambapo janga la picha za ponografia zimezagaa kote ulimwenguni. Ni vigumu kiziepuka. Ponografia inalenga sehemu ya uhalisi wako ambao kwayo kuna uwezo wa kuumba uhai.

Kujiingiza katika ponografia kunakupeleka kwenye shida, kuvunjika kwa ndoa, magonjwa, na taabu za aina nyingi. Hamna sehemu yake ambayo haina hatia. Kuzikusanya, kuzitazama au kuzibeba kwa jinsi yoyote ni kama kumweka nyota hatari kwenye mkoba wako. Kunakuweka kwenye mfano wa kuumwa na nyoka mwenye sumu kali. Mtu anaweza kuelewa kwa urahisi, na ulimwengu ukiwa kama ulivyo, unaweza bila kujua kujingiza ndani yake, kuzisoma au kuzitazama bila kujua matokeo yake mabaya. Kama haya yanaelezea juu yako, nakuonya uache. Koma sasa!

Kitabu cha Mormoni hufunza kwamba wanadamu wote wamefunzwa vyema ili “wajue kati ya mema na maovu” (2 Nefi 2:5). Hiyo inakujumuisha na wewe. Unajua kile kilicho sahihi na kile kilicho kosa. Kuwa makini sana usivuke mstari huo.

Ingawaje makosa mengi yanaweza kuungamwa kwa faragha kwa Bwana, kuna makosa mengine ambayo yanahitaji zaidi ya hayo ili kuleta msamaha. Kama makosa yako ni makubwa sana, mwone askofu wako. Vinginevyo, kuungama kwa kawaida, kwa faragha na kibinafsi, kutatosha. Lakini kumbuka, ile asubuhi kuu ya msamaha yawezekana isije yote mara moja. Kama mwanzo utajikwaa, usife moyo. Kushinda kuvunjika moyo ni sehemu ya majaribu. Usife moyo. Na kama nilivyoshauri awali, mara unapotubu na kuziacha dhambi zako, usitazame nyuma.

Mwokozi Aliteseka kwa Ajili ya Dhambi Zetu

Bwana yupo daima. Yeye ameteseka na kulipa adhabu ikiwa uko tayari kumpokea Yeye kama Mkombozi wako.

Kama wanadamu, sisi hatuwezi, kwa kweli hatuwezi, kufahamu kikamilifu jinsi Mwokozi alivyotimiza dhabihu Yake ya kulipia dhambi. Lakini kwa sasa jinsi gani si muhimu kama kwa nini ya kuteseka Kwake. Kwa nini alifanya hivyo kwa sababu yako, yangu, wanadamu wote? Yeye alifanya hivyo kwa sababu ya upendo wake kwa Mungu Baba na wanadamu wote. “Hakuna mtu aliye na upendo kumshida huyu, kwamba autoe uhai wake kwa sababu ya marafiki zake” (Yohana 15:13).

Katika Gethsemane, Kristo alienda kando mbali kidogo na Mitume Wake ili kuomba. Kile kilichotokea ni zaidi ya uwezo wetu kuelewa! Lakini tunajua kwamba alikamilisha Upatanisho. Yeye alikuwa tayari kujichukulia juu Yake makosa, dhambi na hatia, hofu na uonga wa ulimwengu wote. Aliteseka kwa sababu yetu ili kwamba sisi tusipate kuteseka. Watu wamepata mateso na kufa kifo cha maumivu makali, kifo kibaya. Lakini kuteseka Kwake kunapita mateso yote.

Katika umri wangu, nimepata kujua maumivu ya kimwili ni nini, na siyo mzaha! Hakuna mtu yeyote aepukae katika maisha haya bila kujifunza kitu kimoja au viwili kuhusu mateso. Lakini kuteseka kwake yeye binafsi ambako siwezi kustahamili ndipo ninapokuja kujua kwamba mimi nimesababisha mtu mwingine ateseke. Ndipo basi ninapopata kuona kidogo tu kuteseka kwa Mwokozi alikopata katika Gethsemane.

Kuteseka Kwake ni tofauti na kule kwingine kote kabla au tangu kwa sababu Yeye alijichukulia juu Yake adhabu zote ambazo ziliwekwa kwa ajili ya familia ya mwanadamu. Tafakari haya! Yeye hakuwa na deni la kulipa. Hakutenda kosa lolote. Hata hivyo, jumla ya hatia zote, huzuni na hofu, maumivu na kufedheheshwa, mateso yote ya kiakili, mhemko, na ya kimwili yanayojulikana na mwanadamu—Yeye aliyapata yote. Kumekuwa na Mmoja tu katika historia ya mwanadamu ambaye alikuwa bila dhambi, aliyefuzu kujibu kwa ajili ya dhambi na makosa ya wanadamu wote na kupona uchungu ambao unaambatana na kuzilipia.

Aliutoa uhai Wake na kimsingi alisema, “Ni mimi nichukuae juu yangu dhambi za ulimwengu” (Mosia 26:23). Alisulubiwa; Akafa. Hawangeweza kuuchukua uhai Wake kutoka Kwake. Yeye alikuwa radhi kufa.

Picha
Jesus Christ and the two thieves depicted during the Crucifixion. The Apostle John is standing below the cross of Christ. Mary, the mother of Christ is standing beside John. Two other women are kneeling at the base of the cross. There are Roman soldiers and Jews standing in the background.

Msamaha Kamili Unawezekana

Kama ulijikwaa au hata kupotoka kwa muda, kama utahisi kwamba adui amekukamata mateka, unaweza kusonga mbele kwa imani na usihangaike kule na huko katika ulimwengu tena. Kuna wale waliosimama tayari kukuongoza tena kwenye amani na usalama. Hata neema ya Mungu, kama ilivyoahidiwa katika maandiko, huja “baada ya yote tunayoweza kufanya” (2 Nefi 25:23). Uwezekano wa haya, kwangu, ni ukweli wenye kustahili kuujua.

Naahidi kwamba asubuhi angavu ya msamaha yaweza kuja. Kisha “amani ya Mungu, inayoshinda uelewa wote” (Wafilipi 4:7) itakuja katika maisha yako tena, kitu kama vile machweo, na wewe, kama vile Yeye “hamtakumbuka dhambi zenu tena kabisa” (Yeremia 31:34). Je! Utajuaje? Utajua! (Ona Mosia 4:1–3.)

Hayo ndiyo niliyokuja kuwafundisha ninyi mnaofadhaika. Yeye ataingilia kati na kutatua matatizo ambayo wewe hauwezi kutatua, lakini wewe utahitajika kulipia gharama. Haiwezekani kufanyika bila kutenda hivyo. Yeye ni mtawala mkarimu sana kwa hivyo Yeye daima atalipa gharama inayohitajika, lakini Yeye anakutaka wewe ufanye kile uwezacho kufanya, hata kama ni uchungu.

Mimi nampenda Bwana, na nampenda Baba ambaye alimtuma Yeye. Mizigo yetu ya kufa moyo, dhambi na hatia inaweza kuwekwa mbele Zake, na kwa masharti Yake ya ukarimu, kila kitu katika akaunti kinaweza kutiwa alama “kimelipwa kabisa.”

“Njoo sasa, natushauriane pamoja, asema Bwana: ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu sana, zitafanywa nyeupe kama theluji; ijapokuwa ni nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” Hivi ndiyo, Isaya aliendelea, “kama u tayari na ni mtiifu” (Isaya 1:18–19).

Picha
Jesus Christ with a woman who is wearing a red robe.

Njoo Kwake

Maandiko “Jifunze hekima katika ujana wako; naam, jifunze katika ujana wako kuzishika amri za Mungu” (Alma 37:35) ni mwaliko unaoambatana na ahadi ya amani na ulinzi dhidi ya adui. “Na mtu asipuuze ujana wako; bali uwe mfano kwa waaminio, katika maneno, katika mazungumzo, katika hisani, katika roho, katika imani, katika utakaso” (1 Timotheo 4:12).

Usitarajie kwamba mambo yote yataenda sambamba maisha yako yote. Hata wale wanaoishi kama wanavyostahili, mara nyingine huwa ni kinyume. Kabiliana na kila changamoto ya maisha kwa mtazamo na uhakika, na utakuwa na amani na imani ya kukuhimili sasa na siku zijazo.

Kwa wale ambao hawajapata bado baraka zote mnazohisi mnataka na ambazo mnahitaji kuwa nazo, naamini kwa dhati kwamba hakuna uzoefu au nafasi muhimu ya ukombozi na uokovu watakayo nyimwa wale ambao wanaishi kwa uaminifu. Bakini kuwa wenye kustahiki; kuweni na matumaini, subira, na wenye kusali. Mambo yana njia ya kurekebika. Kipawa cha Roho Mtakatifu kitakuongoza na kitayaelekeza matendo yako.

Kama wewe ni mmoja wa wale wanokabiliwa na hatia, tamaa, au huzuni kama matokeo ya makosa uliyofanya au Baraka ambazo bado hazijaja, soma mafundisho yanayotuliza yanayopatikana katika wimbo “Njoo kwa Yesu”:

Njooni kwake Yesu, ninyi muliolemewa na mizigo,

Mliochoshwa na kuzirai, na dhambi kudhulumiwa.

Atakuongoza salama hadi huko mbinguni

Ambapo wote wanaomwamini wanaweza kupata pumziko.

Njooni kwake Yesu, Yeye milele atakusikiliza,

Ingawa katika giza umepotea.

Upendo wake utakukuta na kwa upole kukuongoza

Kutoka giza la usiku hadi katika mwangaza.

Njoo kwake Yesu, hakika atakusilikiza,

Kama wewe kwa upole utaomba upendo wake.

Oh, haujui kwamba malaika wako karibu nawe

Kutoka makao mema juu?1

Mimi nadai, pamoja na Ndugu zangu Mitume, kuwa ni shahidi maalum wa Bwana Yesu Kristo. Ushuhuda huu unaimarishwa kila mara ninapohisi ndani yangu au kwa wengine athari ya utakaso wa dhabihu Yake takatifu Ushuhuda wangu na ule wa Ndugu zangu, ni wa kweli. Tunamjua Bwana. Yeye si mgeni kwa manabii, waonaji, na wafunuzi Wake.

Ninaelewa kwamba wewe si mkamilifu, lakini unasonga mbele kwenye barabara hiyo. Kuweni na ujasiri. Mjue kwamba yeyote aliye na mwili ana uwezo juu ya yule asiye nao.2 Shetani alinyimwa mwili; kwa hivyo ukikabiliwa na majaribu, jua kwamba wewe unayashinda majaribu hayo yote kama utatumia haki ya kujiamulia aliyopewa Adamu na Hawa katika bustani na kurithishwa kwa kizazi hiki.

Na kama mtatazama mbele kwa tumaini na hamu ya kutenda kile ambacho Bwana angependa mfanye—hayo ndio yote yanayotarajiwa.

Muhtasari

  1. Ona “Come unto Jesus,” Hymns, no. 117.

  2. Ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 211.