2018
Klabu ya Kusoma Kitabu cha Mormoni
Oktoba 2018


Klabu ya kusoma Kitabu cha Mormoni

Jiunge kwa kusoma Kitabu cha Mormoni! Unaweza kukisoma mwenyewe, na familia yako, au na rafiki yako. Kisha tutumie picha yako ukisoma Kitabu cha Mormoni na tuambie kuhusu kitu ulichojifunza au hadithi yako uipendayo toka Kitabu cha Mormoni. Tuma kupitia liahona.lds.org (bonyeza “Tuma Makala”).

Picha
Book of Mormon Reading Club

Andiko takatifu la mwezi huu: Moroni 10:4

“… na ikiwa mtauliza na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.”

Hadithi niipendayo toka Kitabu cha Mormoni inapatikana katika 3 Nefi 17, na ni kuhusu Yesu akiwabariki watoto. Ninaipenda hadithi hii kwa sababu inatuambia jinsi gani Yesu na Baba wa Mbinguni wanavyotupenda. Ninaweza kujitambua nikiwa na watoto, na kuvuta taswira ya kuwepo pale nikiwa nimesimama.

Barbora J., miaka 11, Jamhuri ya Czech

Ninakipenda Kitabu cha Mormoni kwa sababu ni kitabu cha kweli. Kimeandikwa na manabii. Kinanisaidia kuchagua kilicho sahihi, na ninapokuwa na matatizo, kinanisaidia. Ninakiamini.

Jason S., miaka 10, Maharashtra, India