2018
Sala Kwenye Korongo
Oktoba 2018


Sala Kwenye Korongo

Picha
Canyon Prayer

Mwaka jana nilikwenda kupanda mlima pamoja na baba yangu na kaka yangu. Tulienda ndani sana kwenye korongo. Punde tulianza kutafuta barabara pembeni ya korongo. Tuliona mapango makubwa na alama elekezi. Tulipanda zaidi na zaidi juu ya miamba ambayo ilikuwa si imara na miinuko mikali.

Baada ya muda tulikuwa tumepotea kabisa. Hatukujua ni njia gani tungeweza kutumia ili kufika chini kwenye korongo. Tulikwama katikati, tukipoteza uono wa kote juu na chini ya korongo. Nilianza kuchanganyikiwa sana. Sikujua wapi pa kwenda, hali kadhalika baba yangu!

Giza lilikuwa linaingia na baridi ilianza, na hatukuwa karibu sana kutoka kwenye korongo. Nilijua kwamba Baba wa Mbinguni alijua ni njia ipi ya kutokea.

Nilisema, “Kama tunataka kutoka humu, tunahitaji kusali!” Hivyo sote watatu tukapiga magoti na kusali, tukimwomba Baba wa Mbinguni atuongoze kutoka kwenye korongo.

Wakati tulipoanza kutembea, hisia iliniambia kwamba nitakapoona mti mrefu mnyoofu, sina budi kupinda kushoto. Baada ya kupinda kushoto, nililiona gari letu. Nilijua kwamba Baba wa Mbinguni alitusaidia kutoka kwenye korongo. Baba wa Mbinguni alijibu sala yetu, na tulitoka nje salama—punde tu jua lilipokuwa likizama.

Nina shukrani sana kwa sababu ya nguvu ya sala na kwa sababu ya sikio sikivu la Baba wa Mbinguni.