2018
Ukurasa Wetu
Oktoba 2018


Ukurasa Wetu

Picha
Our Page
Picha
Ayana

Ninapokwenda kanisani, ninahisi Roho wa Mungu na upendo nilio nao Kwake na kwa Mwokozi wangu, Yesu Kristo. Ninampenda Mwokozi wangu.

Ayana B., miaka 7, Ufaransa

Picha
drawing by Omar

“Rais Monson na washauri wake”

Omar A., miaka 9, Peru

Picha
Aldo

Ninapenda kuwa hekaluni pamoja na familia yangu. Ni mahala pazuri ambapo nitaweza kwenda nikifikisha miaka 12. Ni nyumba ya Bwana.

Aldo C., miaka 10, Mexico

Picha
Allison

Ninafurahia kushiriki injili shuleni pamoja na rafiki zangu, hasa na mvulana ambaye ana shida katika kuzungumza, kuandika, na kusoma. Njia mojawapo ya kushiriki injili kama Yesu Kristo alivyofundisha ni kwa kuwasaidia na kuwatumikia wengine. Kila wakati mwalimu akitupatia kazi ya kufanya katika daftari la mazoezi ya nyumbani, mara zote ninakuwa tayari kumsaidia mvulana huyu. Ninapenda kuwatumikia wengine kwa sababu inanisaidia mimi kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni.

Allison M., miaka 10, El Salvador