2018
“Je, Ninawezaje kumwalika Roho nyumbani kwangu wakati watu wakigombana na kubishana?”
Oktoba 2018


“Je, Ninawezaje kumwalika Roho nyumbani kwangu wakati watu wakigombana na kubishana?”

Picha
young man looking out the window

Sema Samahani

Wakati nimekuwa na mabishano, Nimegundua kwamba kwa kuomba radhi na kukubali kwamba umekosea, hata kama unafikiri au kujua kwamba uko sahihi, husaidia kurudisha amani katika chumba. Kisha toka nje, kaa kimya, badilisha mada, au tafuta kitu cha kukubaliana. Haichukui muda kwa Roho kurudi.

Dylan M., miaka 15, California, Marekani

Penda Tu

Nimegundua kwamba kuonyesha upendo wa kweli kwa familia yangu humwalika Roho kukaa nyumbani mwetu. Nabii aliongea kuhusu upendo kama kichocheo ambacho husababisha badiliko na malhamu ambayo huleta uponyaji wa nafsi. Roho ya upendo huleta usalama na amani nyumbani.

Joseph C., miaka 18, Arizona, Marekani

Zungumza na Familia Yako

Kama wanafamilia yako si waumini wa Kanisa, waambie ni vibaya kiasi gani unajisikia pale wanapobishana na waombe wajirekebishe. Kama hiyo haitasaidia, sali na jaribu tena. Kama ni waumini, wakumbushe kwamba wao ni watoto wa Mungu na kwamba wanatakiwa kuepuka ugomvi.

Carolina S., miaka 19, Goiás, Brazil

Omba kwa ajili ya Roho

Wakati wanafamilia wanapobishana, ni vigumu kuhisi uwepo wa Roho, lakini hii haimaanishi kwamba huwezi kumuhisi kama unastahiki. Sali katika moyo wako kwa ajili ya nyongeza zaidi ya Roho wa Bwana na kuwa makini zaidi katika misukumo inayotumwa kwako. Baba wa Mbinguni anaweza kukusaidia kuhisi amani na kujua ni namna ipi nzuri zaidi ya kurudisha amani katika nyumba yako.

Katie G., miaka 17, Utah, Marekani

Jaribu Kuelewa

Ongea na familia yako kutataua tatizo katika njia ambayo kila mmoja ananufaika, au shiriki andiko takatifu au imba wimbo. Unaweza pia kumwomba Baba wa Mbinguni msaada wa kutatua tatizo. Katika njia hii, kila mmoja atatulia na kuwa na uwezo wa kutatua tatizo bila kuwa na sababu ya kupaza sauti au vurugu. Hakika Roho Mtakatifu atawajaza nyote na amani na kumpa kila mtu hamu ya kutotaka kugombana tena.

Luis F., miaka 14, Playa del Carmen, Mexico