2018
Njia Ambazo Hukuandaa kwa ajili ya Siku Zako Usoni
Oktoba 2018


Njia Ambazo Hukuandaa kwa ajili ya Siku Zako Usoni

Bila kujali kama unaenda chuoni, unatafuta kazi, au unajifunza biashara, unakuza sifa ambayo ni muhimu katika kujenga ufalme wa Mungu.

Picha
paths

Sidhani kama ni ndoto ya msichana yoyote wa miaka 14 kujikuta katika ghala lenye vumbi, akibeba koleo lenye kutu, akisafisha banda la farasi lenye kutoa harufu. Lakini hapo ndipo nilipokuwepo mimi kila baada ya shule mpaka nilipokuwa vya kutosha kupata kazi tofauti.

Hakika haikuwa ni lengo langu kufanya kazi nikiwa shule ya upili, lakini nilielewa kipindi hicho kwamba kama ningetaka kazi ambayo kweli niliipenda—kazi ambayo haikuwa ya kusafisha wanyama—nilihitaji kwenda chuoni, na kwenda chuoni, nilihitaji fedha. Nilijua kwamba kwangu, elimu ilikuwa ni hatua sahihi kuelekea (kwa matumaini) kupata kazi.

Kitu kizuri ni kwamba njia niliyochagua ni moja tu kati ya nyingi ambazo zinaweza kukusaidia kujifunza kufanya kazi na kutimiza mahitaji yako wewe mwenyewe. Hii huitwa kujitegemea kimwili na kiroho. Wakati ukitafakari chaguzi zako, jaribu kuchagua njia ambayo unahisi itakuandaa vizuri zaidi.

Hadithi hizi ni kutoka kwa watu ambao walikuwa wa umri sawa na wako miaka michache tu iliyopita. Kwa kufuata mifano ya hawa vijana wakubwa, unaweza kupata njia yako mwenyewe kuelekea kufanikiwa kujitegemea.

Fikiria Mahitaji Yanayokuzunguka

Na Oudom Piseth, Cambodia

Picha
Oudom

Ili kuweza kufanikisha malengo yangu, kila mara ninajiambia nafsini mwangu kwamba kufanya kazi kwa bidii ni muhimu sana, lakini njia nyingine ya kuwa mjuzi ni kufanya kazi kwa umakini. Baada ya kutoka misheni huko Uingereza, nilirudi Cambodia na kuangalia soko la ajira. Niliangalia vitu kama urefu wa muda wa mafunzo ili kupata kila kazi na gharama ya mafunzo.

Niligundua kwamba mafunzo ya kuwa mratibu wa mauzo wa nguo ni mafupi lakini yenye changamoto, na si watu wengi walikuwa wakiyafanya. Niliona kwamba ilikuwa fursa nzuri na nikaamua kuichukua. Sasa nimemaliza mafunzo na ninafanya kazi kama mratibu wa mauzo kwenye kampuni ya nguo.

Kupata kazi sahihi kunaweza kuwa vigumu sana, lakini nina Mwokozi kunisaidia na kuniinua.

Tumia Elimu Kufungua Milango

Na Iolanda Teixeira, Cape Verde, Afrika

Picha
Iolanda

Mama yangu mara zote alinitia moyo kwa kirai, “Elimu ni ufunguo wa mafanikio.” Nilitaka kuwa na siku za usoni nzuri zaidi kwa ajili yangu na hasa kwa familia yangu, na kufanya hivyo, nilihitaji kuendelea na elimu. Bila kuwa na fedha ya kwenda chuo kwa wakati huo, niliomba ufadhili kuhudhuria shule ya mafunzo stadi kusoma kuhusu mifumo ya tarakilishi na utunzaji wake.

Katika kipindi chote cha masomo yangu nilikumbana na changamoto nyingi, lakini hii haikunizuia kuendelea mbele nikielekeza macho yangu kwenye siku nzuri zijazo. Sala ilinisaidia sana; mara zote ninatafuta ushauri kutoka kwa Bwana. Kila mara nimekuwa mwenye bidii katika masomo yangu, na leo ninabakia mwenye bidii katika kazi yangu, nikitoa kilicho kizuri zaidi kama mtaalamu wa tarakilishi na msaidizi wa masoko.

Fanya Kazi sasa Kuelekea Siku za Usoni Utakazo

Na Ann-Sophie and Lawrence Cavin, Scotland, Uingereza

Picha
Ann-Sophie

Ann-Sophie: Mara zote nilitaka kusoma chuo kikuu, lakini mipango yangu kuhusu nini cha kusoma ilibadilika sana wakati wa ujana wangu. Baada ya kumaliza shule ya upili, nilijitolea kwenye hospitali kwa miezi sita. Tangu hapo nilipenda wazo la kuwa nesi, lakini sikudhani kama ningeweza kuwa hivyo.

Katika darasa la kujifunza kujitegemea kwenye kata yangu, tuliombwa kuchagua kazi ambayo tulipenda kuwa nayo hata kama hatukuwa na vigezo. Nilisali kuhusu nini cha kufanya, na unesi ulikuwa ukinijia kila mara mawazoni mwangu. Niliamua kufuata ushawishi wa Bwana.

Kufuata njia hii hakukuwa rahisi. Kwa kuanza, nilichunguza kuhusu programu ya unesi na nini kingehitajika kwangu katika kuisomea. Nilizungumza na watu ambao walikuwa wamepitia mchakato kama huo. Mara ya kwanza nilipotuma maombi ya programu ya unesi, niliwekwa kwenye kundi la wanaosubiri. Lakini sikukata tamaa; nilituma maombi tena na hatimaye nikapata. Wakati mwingine unahitajika kuwa mvumilivu na kumwamini Bwana kwa maana Yeye ana mpango kwa ajili yako.

Picha
Lawrence

Lawrence: Wakati nilipokuwa mdogo, niliweka lengo la kuja kuwa mzuri niwezavyo bila kujali somo lolote nitakalosoma au kazi nitakayo kuwa nayo. Mara zote nilijaribu kujifunza na kuwa bora kuipa nafsi yangu nafasi nzuri ya kufanikiwa.

Kwa sasa nafanya kazi kama meneja wa kampuni ya nguo, lakini nataka kujiunga na jeshi la polisi. Hapa Scotland, unatakiwa kuishi katika nchi kwa miaka mitatu mfululizo kabla hujaomba kuwa polisi. Kwa kuwa nilikuwa nje ya nchi kwa miaka miwili nikitumikia misheni, ninatakiwa kusubiri kwa miezi michache kabla ya kujiunga.

Ingawa hiki kimekuwa kikwazo kikubwa sana, bado sijakata tamaa. Nina kazi nzuri ya kuitimizia mahitaji familia yangu, na nina fanya kazi kwa bidii kuhakikisha ninapata sifa nzuri kwa ajili ya kazi za siku zijazo.

Kama vijana hawa wakubwa, utagundua kwamba njia tofauti tofauti zinaweza kukuandaa kujitunza wewe mwenyewe na familia yako ya siku zijazo. Kwa lengo hilo mawazoni, unaweza kupanga kwa ajili ya mafanikio. Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha “Acha tufanye vizuri tuwezavyo na kupalilia sifa bora katika kila tufanyalo. Acha tuweke mawazo yetu na miili yetu katika fursa tukufu kwa kazi ambayo huletwa na kila siku iliyo mpya” (“Kanuni Mbili kwa Uchumi Wowote,” mkutano mkuu wa Okt. 2009). Unapozingatia sasa katika kujifunza na kufanya kazi, utatengeneza tabia ambazo zitakusaidia kuhisi ujasiri zaidi kuhusu siku zijazo.