2021
Kuileta Sayuni
Septemba/ Oktoba 2021


Kuileta Sayuni

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho walivyobarikiwa na injili ya urejesho, tumeitwa kuimarisha Kanisa na kujenga Sayuni.

Picha
map of the world

Picha ya ramani kutoka Getty Images

Katika hisitoria yote, watu wa Bwana wametafuta kuleta mbele jamii ya injili ambapo Anaweza kukaa. Kuwa jamii kama hii ya Watakatifu, tunapaswa kujifunza kutakasa na kuuganisha mioyo na akili zetu, na kufanya haki bila mabishano na ugomvi, na kukaa katika utakatifu pasipo kuwepo na masikini kati yetu (ona Musa 7:18).

Kwa mfano, baada ya John na Maria Linford kujiunga na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Gravely, Uingereza, mnamo 1842, John alikuwa Rais wa tawi. Ndugu na marafiki, hata hivyo, hawakushiriki furaha akina Linford waliyoipata katika Urejesho. Ikiwa wangeshindwa kumshawishi John kuachana na dini yake mpya, hapo wange “msababishia njaa” kwa kususia biashara yake ya kutengeneza viatu.

Mnamo 1856 Mfuko Endelevu wa Uhamiaji ulimpatia John na Maria nafasi ya kuhamia Salt Lake Valley. Walisafiri kuelekea New York pamoja na wana wao watatu. Kutoka hapo walisafiri hadi mji wa lowa, lowa, ambako waliondoka Julai 1856 akiwa mgonjwa na dhaifu kwa kutumia mkokoteni wa kundi la James G.Willie.

Mapema mnamo Oktoba 21, karibu na kingo za Mto Sweetwater huko Wyoming, John aliongea maneno yake ya mwisho.

“Ninafuraha tulikuja,” alimwambia Maria alipomuuliza kama alijuta kwa kuondoka Uingereza. “Mimi sitakuwa hai kufika Salt Lake, lakini wewe na wavulana mtafika, na sijutii yale yote tuliyoyapitia kama wavulana wetu wataweza kukua na kulea familia zao katika Sayuni.”1

Sayuni ni nini?

Picha
group of pioneers

Mada chache nje na kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo zimewahamasisha manabii na Watakatifu wa zamani na wa sasa kuliko kusanyiko la mwisho la nyumba ya Israeli na kuijenga Sayuni kwa maandalizi ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.2

Kwa nini Sayuni ni muhimu kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho—wa kale na wa sasa, popote pale watu wa Bwana wanapatikana?

Mzee Bruce R. McConkie (1915–85) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitamka, “Kutoka siku za Adamu hadi nyakati za sasa—Wakati Bwana alipokuwa na watu wake; wakati walikuwepo watu waliotii sauti yake na kushika amri zake; wakati Watakatifu wake wamemtumikia kwa lengo moja la moyo—hapo pamekuwepo Sayuni.”3

Maandiko yanaelezea jumuia ya Sayuni. Henoko, nabii mwenye imani kubwa wa nyakati za Nuhu, “alijenga mji ambao uliitwa Mji wa Utakatifu, hata Sayuni” (Musa 7:19). Bwana alikaa hapo na watu Wake, akiwabariki wao na aridhi yao (ona Musa 7:16–18). Bwana akamwabia Henoko, “Tazama, Mimi ndimi Mungu; Mtu wa Utakatifu ndilo jina langu” (Musa 7:35).

Matamanio ya Sayuni ni kuanzisha sehemu iliyoungana kiimani yenye msingi katika kanuni za mbingu ya selestia, ambapo watu wa Mungu wanaweza kutembea Naye na Mungu Mwenyewe anaweza kuwa na makao.

Kitabu cha Mormoni kinashuhudia kwamba baada ya Mwokozi aliyefufuka kutembelea Dunia Mpya, “watu wote waliongoka katika Bwana, juu ya uso wote wa nchi. …

“Na walikuwa na vitu vyote kwa usawa miongoni mwao; kwa hivyo hakukuwa na tajiri na masikini, wafungwa na walio huru, lakini wote walifanywa huru, na washiriki wa karama ya mbinguni. …

“Na ikawa kwamba hakukuwa na ubishi katika nchi, kwa sababu ya mapenzi ya Mungu ambayo yaliishi katika mioyo ya watu” (4 Nefi 1:2, 3, 15).

Kujihami kwa Utakatifu na Nguvu

Siku za Henoko zilikuwa siku za vita, umwagaji damu, hofu, giza, na chuki—wakati “nguvu za Shetani zilikuwa pote juu ya uso wa dunia “ (Musa 7:24; ona pia msitari 16, 17, 33). Hata Henoko alikuwa mwaminifu, na Bwana alimuita kupaza sauti kwa ajili ya toba.

Bwana alimwambia Henoko aina ile “taabu nyingi” (Musa 7:61) itatanguliwa na Ujio Wake wa Pili. “Kama vile niishivyo, hata hivyo nitakavyokuja katika siku za mwisho, katika siku za uovu na kulipa kisasi, kutimiza kiapo ambacho nimekuapia juu ya watoto wa Nuhu” (Musa 7:60)

Kwa siku zetu, Rais Russell M. Nelson hivi karibuni alisema, “Nalitizama kwa sasa janga la [COVID-19] kama mojawapo ya maradhi mengi ambayo hushambulia dunia, ikijumuisha chuki, machafuko ya kijamii, ubaguzi,vurugu, kutokuwa waaminifu, na kukosa ustaraabu.”4 Na bado, tunao uhakika wa kinabii. Rais Nelson pia amesema:

“Tunaishi katika siku ambazo ‘babu zetu wamekuwa wakizisubiri kwa shauku kubwa.’ [Mafundisho na Maagano 121:27.] Tumekaa viti vya mbele kushuhudia mubashara kile nabii Nefi alichokiona katika ono tu, kwamba ‘nguvu ya mwanakondoo wa Mungu’ itawashukia watu wa agano wa Bwana, ambao walitawanyika kote usoni mwa dunia; na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu.’ [1 Nefi 14:14.]

Ninyi, kaka zangu na dada zangu, ni miongoni mwa wale wanaume, wanawake, na watoto ambao Nefi aliwaona.”5

Mwaliko wa kuwakusanya na kuwabariki wale wote walio katika pande zote za pazia, kujenga Sayuni, na kuiandaa dunia kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi inatujumuisha sisi wote. “Kati ya watu wote ambao wamewahi kuishi katika sayari ya dunia” alisema Rais Nelson, “sisi ni moja ya wale tunaopata nafasi ya kushiriki katika tukio hili la mwisho, la mkusanyiko mkuu.”6

Je! Tunafikaje Kule?

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho tukibarikiwa na injili ya urejesho, sisi “tunaitwa kufanya kazi katika shamba, la [Bwana] na kujenga Kanisa, [Lake] na kuilstawisha Sayuni” (Mafundisho na Maagano 39:13). Kazi hiyo inahitaji upendo, umoja, huduma, dhabihu na utiifu.

Picha
group of women outside a church

“Wakati watu wanapompenda Mungu kwa mioyo yao yote na kwa haki wakijitahidi kuwa kama Yeye, kunakuwa na ugomvi na malumbano machache katika jamii. Kuna umoja zaidi,” alisema Mzee Quentin L Cook wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Aliongeza: “Umoja ni … neno pana, lenye mambo mengi lakini kwa hakika ni mfano wa amri kuu ya kwanza na ya pili ya kumpenda Mungu na kuwapenda wenzetu. Linaashiria watu wa Sayuni ambao mioyo na akili zao ‘vimeunganishwa pamoja katika umoja’ [Mosia 18:21].”7

Kwa upendo huo na umoja, tunatekeleza imani kuwa karibu na Upatanisho wa Mwokozi, ambao unaweza kutubadilisha kadiri tunavyotakasa mioyo yetu na maisha (ona Mosia 3:19; Mafundisho na Maagano 97:21). Tunawakusanya wale walio na utashi wa kuja kwa Bwana katika haki. Kupitia ibada takatifu na kanuni za selestia, tunaalika nguvu za kiungu katika maisha yetu (ona Mafundisho na Maagano 105:5). Ikitakaswa na agano linalotoka kwa Mungu na kila mmoja, tunajenga Sayuni na kuandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili.

“Hisani ni upendo kamili wa Kristo,” alisema Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza. “Na ni imani katika Yeye na matokeo kamili ya Upatanisho Wake usio na mwisho ambavyo vitakustahilisha wewe, na wale unaowapenda na kuwatumikia, kwa ajili ya zawadi ya mbinguni ya kuishi katika ujamaa wa Sayuni iliyotazamiwa na kuahidiwa.”8

Jiandae kwa ajili ya Siku Zijazo

Picha
group of young men sitting in a Church class

Manabii wa sasa hufundisha kwamba kuja kwa Mwokozi ni swala la mtu binafsi kujitolea, sio sehemu iliyopangwa.

“Katika siku za mwanzo za Kanisa, uongofu mara nyingi ulimaanisha pia uhamiaji,” Rais Nelson amaeeleza. Lakini sasa kukusanyika kunafanyika katika kila taifa. Bwana ameagiza kuanzishwa kwa Sayuni kila eneo ambako amewapa Watakatifu Wake uzaliwa wao na utaifa.”9

Kadiri tunavyokumbatia changamoto na baraka za kujenga Sayuni katika familia zetu, matawi, kata, vigingi, na jamii tunatizama na John na Maria Linford kuelekea pale wototo na wajukuu wetu “wanaweza kukua na kulea familia zao katika Sayuni” katika kila taifa, jamaa, na ndimi.

Kadiri tunavyomtafuta Bwana na haki Yake, tunasali “ili ufalme wake uweze kuenea juu ya dunia, ili wakazi wake waweze kuupokea, na kujitayarisha kwa ajili ya siku zijazo, siku ambazo Mwana wa Mtu atashuka kutoka mbinguni, aliyevikwa katika mng’aro wa utukufu wake, kukutana na ufalme wa Mungu ambao umewekwa duniani” (Mafundisho na Maagano 65:5).

Muhtasari

  1. Ona Andrew D. Olsen, The Price We Paid: The Extraordinary Story of the Willie and Martin Handcart Pioneers (2006), 45–46, 136–37.

  2. Ona Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli” (worldwide youth devotional, Juni 3, 2018), HopeofIsrael.ChurchofJesusChrist.org.

  3. Bruce R. McConkie, “Come: Let Israel Build Zion,” Ensign, Mai 1977, 116–17.

  4. Russell M. Nelson, katika Sarah Jane Weaver, “Rais Nelson anatualika Sisi Kutoa Shukrani,” Nov. 20, 2020, thechurchnews.com.

  5. Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 88.

  6. Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli,”

  7. Quentin L. Cook, “Mioyo Iliyounganishwa katika Haki na Umoja,” Liahona, Nov. 2020, 18, 19

  8. Henry B. Eyring, “Akina Dada katika Sayuni,”Liahona, Nov. 2020, 69.

  9. Russell M. Nelson, “Kusanyiko la Israeli Iliyotawanyika,” Liahona, Nov. 2006, 81