2021
Kuwasaidia Wengine Kujiandaa Kwa ajili ya Mahitaji Yasiyotarajiwa
Septemba/ Oktoba 2021


Kanuni za Kuhudumu

Kuwasaidia Wengine Kujiandaa Kwa ajili ya Mahitaji Yasiyotarajiwa

Kama akina kaka na dada wahudumiao, tunaweza kuwasaidia kaka na dada zetu kujiandaa kwa ajili ya dunia isiyotabirika.

Picha
a mother and her toddler son planting an indoor garden

Picha kutoka Getty Images

Majanga makubwa, majanga ya asili, anguko la kiuchumi, misukosuko ya kisiasa, na migogoro ya ghasia—dunia imeona mengi ya haya katika mwaka uliyopita. Kwa nyongeza ya matukio makubwa haya, tunakabiliana pia na changamoto zisizotarajiwa katika maisha yetu binafsi, kama vile magonjwa, kupoteza kipato, talaka, na mengine mengi.

Juhudi zetu kujiandaa kwa ajili ya yasiyotarajiwa inaweza kutoa usalama na ulinzi kwa ajili yetu na wengine. Tunaweza kufanya nini kama kaka na dada wahudumiaji ili kuwasaidia wale tuwapendao wanaosumbuliwa na dhoruba wasizotarajia katika maisha yao?

Carlomagno Aguilar wa Angeles, Philippines, hutoa mfano mmoja. Alipojua eneo lake linaweza kuwekwa chini ya karantini sababu ya janga la COVID-19, aliwahi kununua mahitaji—ingawa orodha yake ilikuwa tofauti na za wale waliomzunguka. Alikuwa na mpango wa kujiandaa—kununua mbegu na mbolea kwa ajili ya bustani ya nyumbani kwake.

Picha
video still of man teaching about growing food

Carlomagno Aguilar alianza idhaa ya mtandaoni kufundisha kuhusu kilimo cha mjini.

Katika jitihada za kujitegemea zaidi, Carlomagno amekuwa mkulima wa mjini kwa miaka mingi. Huwahudumia pia majirani zake, kwa vyote kwa kuwagawia mazao kutoka kwenye bustani yake na kuwafundisha kuzalisha chakula chao wenyewe. Vile vile alianzisha idhaa ya mtandaoni ambapo vidokezo na mafundisho yake vinapatikana kwa kila mmoja, akiwasaidia kaka na dada zake kuweza kujitegemea na kujiandaa kwa ajili ya wakati ujao.

Askofu W. Christopher Waddell, Mshauri wa Kwanza katika Uaskofu Simamizi, alifundisha: “Tunapokumbatia kanuni za kiroho na kutafuta uongozi wa kiroho kutoka kwa Bwana, tutaongozwa kujua matakwa ya Bwana, binafsi na kama familia, na kwa njia iliyo bora kutumia kanuni muhimu za utayari wa kimwili. Hatua muhimu zaidi ya zote ni kuanza” (“Palikuwepo na Mkate,” Liahona, Nov. 2020, 44–45).

Kusaidia kila mmoja kuwa tayari katika dunia hii isiyotabirika ni jambo la msingi, kuweka njia ya kuonyesha upendo wa Kristo. Acha tusaidiane sisi kwa sisi kuchukua “hatua muhimu” ya kuanzia.

Mapendekezo kwa ajili ya Kuwasaidia Wengine

Kama kawaida, kuhudumia huanza na sala ya kuzingatia na kushauriana kwa pamoja. Mapendekezo yafuatayo yanaweza kukusaidia kufikiria namna ya wewe au wale unaowahudumia wangeanza kujiandaa kukabiliana na changamoto zisizotarajiwa.

  1. Fikiria kitakatifu . Tunaweza kujiandaa katika njia nyingi kwa maeneo tofauti ya maisha yetu. Ni muhimu kuhifadhi na kuzalisha chakula kadiri unavyoweza, jiandae kifedha, jenga uthabiti wa mawazo, na kuweka mipango kwa hali za dharura.

  2. Jadili changamoto ambazo zina uwezekano wa kutokea pale unapoishi na namna ya kuzikabili. Sehemu tofauti duniani zina changamoto za kipekee. Ikiwa unaishi mahala ambapo tetemeko ni kawaida, jadili jinsi unavyoweza kuandaa nyumba yako kukusaidia kukaa salama, kama vile kupata fanicha nzito ukutani. Au kama unaishi mahala ambapo vimbunga ni kawaida, jadili namna ya kukabiliana na hali hiyo, kama vile kuacha redio wazi ili kupata habari au kuhamia katika nyanda za juu.

  3. Jadili jinsi ya kuunda mfuko wa dharura. Kuweka pesa kunaweza kukusaidia ikiwa utapoteza kazi au kuwa na matumizi zaidi ambayo hukutegemea. Zungumza namna ya kuweka pesa, kama vile kwa kuanza kidogo kidogo kuweka kidogo kila wakati unapolipwa mpaka unafikia lengo lako.

  4. Kusanya mahitaji kwa ajili ya dharura katika chombo kimoja. Kuwa na chombo cha dharura kunaweza kukusaidia kuwa tayari ikiwa unahitaji kuondoka nyumbani kwa muda mfupi. Fanyeni kazi pamoja kufikiri na kusanya vitu vinavyohitajika. Hii inaweza kufanyika kwa kipindi cha muda na haihitaji kufanyika kwa mara moja. Fikiria sehemu ya hifadhi, chakula na maji, mahitaji ya matibabu, mwanga, mawasiliano, nyaraka muhimu, pesa, nguo za kubadilisha, zana za burudani na faraja (michezo, vitabu, wanasesere kwa ajili ya watoto,) na mahitaji mengine.

  5. Jenga urafiki na mtu unayemhudumia. Ni muhimu kuwa na ujuzi imara wa kuiga kwa ajili ya kumudu misukumo inayokuja na ugumu. Moja ya ujuzi huu ni kuwa na mahusiano mazuri. Kadri unavyoimarisha urafiki wako na mtu huyo, utakuwa unawasaidia kutengeneza mfumo wa usaidizi.

  6. Zungumza kuhusu uhifadhi wa chakula. Inaweza kusaidia kuwa na chakula cha ziada kwa ajili ya darura. Peaneni changamoto kuanza kwa kujenga mipango ya muda mfupi ya mahitaji ambayo unatumia na kujaza katika mapishi yako ya kila mara. Kisha anza kufanya kazi mipango ya muda mrefu ya kukusanya chakula kikuu. Kama huna nafasi kubwa ya kuhifadhi chakula au kama unazuiliwa na sheria kuweka chakula kingi, weka tu kile kinachoendana na mazingira yako.