2021
Baraka zipi huzipata wasafi katika moyo?
Septemba/ Oktoba 2021


Njoo, Unifuate

Baraka zipi huzipata wasafi katika moyo?

Mafundisho na Maagano 94–97

Picha
men working on Kirtland Temple

Kielelezo na Dan Burr

Katika vifungu hivi tunajifunza kuhusu amri za Bwana kwa Watakatifu wa zamani kujenga hekalu.

“Wasafi Moyoni … Watamwona Mungu”

Katika kifungu cha 97, Bwana anaahidi kwamba ikiwa Watakatifu watajenga hekalu na kuliweka safi, “na wote wasafi moyoni watakaoingia ndani yake watamwona Mungu” (aya 16). Baada ya kunukuu aya katika mazungumzo ya mkutano mkuu, Mzee David B. Haight (1906–2004) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema:

“Nikweli kwamba baadhi hakika wamemwona Mwokozi, ila mmoja anaporejea kwenye kamusi, anajifunza kwamba kuna maana nyingi za neno ona, kama vile kuja Kwake, kumjua Yeye, kumtambua Yeye na kazi Zake, kuelewa umuhimu Wake au kumuelewa Yeye.

“Mwangaza huu wa kimbingu na baraka vinapatikana kwa kila mmoja wetu.”1

Ni kwa njia gani umeona Mungu akijidhihirisha Mwenyewe katika hekalu?

Shughuli ya Kusoma Maandiko

Maandiko haya yanafafanua baadhi ya baraka nyingine ambazo huja kwa wenye moyo safi.

Mjadala

Je, ni jambo gani sana sana unafurahia kwa kuweza kuhudhuria hekaluni?

Muhtasari

  1. David B. Haight, “Temples and Work Therein,” Ensign, Nov. 1990, 61.