2021
Kutambua Mazuri ndani Yetu
Septemba/ Oktoba 2021


Vijana Wakubwa

Kutambua Mazuri ndani Yetu

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuelezea kipawa cha utambuzi? Mpaka hivi karibuni, nilikuwa na kosa mojawapo ya madhumuni muhimu ya kipawa hiki.

Picha
woman looking away against background of sea and sky

Vielelezo vya Picha kutoka Getty Images

Kwa maisha yangu yote, nimefafanua kipawa cha utambuzi kama kuwa na uwezo wa kujua mema kutoka kwenye mabaya, ukweli kutoka kwenye makosa. Wakati hii ikiwa ni sehemu ngumu ya kipawa, hivi karibuni nilijifunza kuna zaidi kwayo.

Nilipata hazina katika tanbihi ya hotuba iliyotolewa katika mkutano mkuu wa Aprili 2020. Msemaji alimnukuu Rais Stephen L Richards (1879–1959), Mshauri wa Kwanza wa zamani katika Urais wa Kwanza, ambaye alisema, “Aina ya kiwango cha juu cha utambuzi ni ile ambayo inapokea katika wengine na kufumbua kwa ajili ya uzuri wa asili yao, urithi mzuri ndani yao.”1

Hii haionekani kama ushairi?

Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kufumbua uzuri asili ndani ya wengine. Ukweli wa kauli hii ulikuwa mzuri kiasi kwamba nilitaka kujifunza zaidi. Niligundua kwamba Mzee David A. Berdnar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili pia alifundisha kwamba baraka ya utambuzi inatusaidia sisi “kutafuta na kuleta mazuri ambayo yanaweza kufichwa ndani yetu sisi.2

Tangu ugunduzi huu, nimekuja kuelewa kipawa hiki cha utambuzi ni muhimu kiasi gani. Tunahitaji kutafuta uzuri bora ndani yetu wenyewe ili kuweza kuuendeleza. Kadri tutakavyofanya, tutahisi na kutenda zaidi kama watoto wa Mungu tulio (ona Zaburi 82:6; Mosia 5:7; Moroni 7:19).

Kwa hiyo tunawezaje kuanza kutafuta uzuri ndani yetu? Hapa kuna njia chache za kuweza kuanza.

Zingatia katika Kutumia Uwezo Wako Kubariki Wengine

Ni ukweli wa kimafunzo kwamba kila mmoja anazo baraka kutoka kwa Mungu (ona Mafundisho na Maagano 46:11)—na sio bure kufikiri kuhusu wao. Kwa kweli, Bwana ametuomba sisi! Maandiko yanatufundisha sisi kutafuta “kwa bidii vipawa vizuri, daima kukumbuka kwa kile walichopewa” (Mafundisho na Maagano 46:8; msisitizo umeongezwa).

Kadri tunapopata uelewa zaidi wa vipawa vyetu au karama, tunapaswa kutafuta njia kuzitumia kutumikia wengine.

Njia mojawapo ya kutambua vipawa vyako ni kwa kumuuliza mtu unaye mwamini! Waulize nguvu zako ni zipi. Ikiwa uko kama mimi, unaweza kufikiri kwamba hilo linaonekana baya. Ila kumbuka, hii sio kuhusu ubatili; nikuhusu kutafuta kile ambacho tabia ya mtu binafsi au sifa unazoweza kutoa kwa kaka na dada zako wa duniani (ona Mosia 8:18).

Kwa mfano, jirani mwema aliwahi siku moja kuniambia kwamba nina kipawa cha kusaidia watu kujisikia vizuri. Badala ya kuyadharau maoni kama njia pekee ya sifa ya upole, nilianza kutizama hiki kipawa ndani yangu. Kadri nilivyofanya hivyo, niligundua kwamba Baba wa Mbinguni angeweza kunisaidia kutumia ujuzi wangu wa kijamii kufanya urafiki na wengine na kubariki maisha mengi zaidi kuliko yangu mwenyewe.

Kwa kutambua vipawa vyako, unaweza kuchagua kwa umakini kuvitumia kubariki wengine (ona Mafundisho na Maagano 82:18).

Jifunze Baraka Yako ya Kipatriaki

Picha
a young woman reading her patriarchal blessing

Picha na Judith Ann Beck

Baraka za Kipatriaki vile vile ni chanzo kizuri kwa ajili ya kuona vipawa tofauti alivyotupa Mungu. Mzee Larry R. Lawrence, mshiriki wa kudumu wa akidi ya Sabini, alisema: “Roho anaweza kutuonyesha udhaifu wetu, lakini Ana uwezo wa kutuonyesha uwezo wetu. … Tunaposoma baraka zetu za kipatriaki, tunakumbushwa kwamba Baba yetu wa Mbinguni anajua uwezo wetu mtakatifu.”3

Kujifunza baraka zako za kipatriaki hukusaidia wewe kukuza tabia ambazo zinaweza kukusaidia kufikia uwezo wako.

Kwangu mimi, huwa nafikiria aina ya mama natamani kuwa siku moja. Bila kutambua, nilishikwa na fikra kwamba mama yuko vizuri, amejipanga, na mrembo—na kwamba wema wake unaonewa kijicho na Usaidizi wa Akina Mama wa Kata yake. Wakati hivi vitu si vibaya, kujifunza baraka zangu za kipatriaki kumenionyesha kwamba Bwana ananijali zaidi kwamba ni mama mwenye upendo na huruma. Kwangu mimi, tabia kama za Yesu Kristo ndizo ambazo napaswa kuziendeleza.

Kumbuka na Tafakari wakati wa sakramenti.

Picha
bread being broken for sacrament

Picha na Jerry Garns

Sakramenti ni wakati wa kufikiria kuhusu Mwokozi. Ni wakati pia kutafakari juu ya maendeleo yako kuelekea kuwa kama Yeye. Kadri unavyojitahidi kugundua tabia zako nzuri za urithi, ukitizama nyuma kila juma kwenye mafanikio yako, uzoefu, na matukio ya kijamii inaweza kukusaidia kuona baadhi ya nyakati ambapo vipawa vyako vilijitokeza.

Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema: “Unapochunguza maisha yako wakati wa ibada ya sakramenti, ninatumai ya kwamba mawazo yako hayatalenga tu kwenye vitu ambavyo hukufanya vyema lakini pia kwenye vitu ambavyo umeweza kufanya vyema—nyakati ambazo umeweza kuhisi ya kwamba Baba wa Mbinguni na Mwokozi walikuwa wamefurahishwa nawe. Unaweza hata kuchukua nafasi wakati wa sakramenti kumuomba Mungu akusaidie uone mambo haya.”4

Hapa kuna baadhi ya maswali ambayo ungeweza kujiuuliza au kumuuliza Mungu wakati wa Sakramenti:

  • Ni kwa jinsi gani nimeweza kumfuata Mwokozi wiki hii?

  • Nani nilimhudumia?

  • Ni wakati gani nilihisi Roho wiki hii? Kwa nini?

  • Ni tabia zipi kama za Kristo najaribu kuzikuza? Nafanya jinsi gani?

  • Je, kuna kitu chochote katika maisha yangu napaswa kusali kwa ajili ya kuomba msaada?

  • Je, kuna mtu yoyote nahitaji kumsamehe?

  • Ni tatizo gani moja, kubwa au dogo, ambalo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo alinisaidia katika juma hili?

Kutafakari uzuri wa Mungu na kutathmini maisha yangu wakati wa sakramenti kuliko kulenga tu kwenye mapungufu na kasoro hunisaidia mimi kuweka imani yangu katika Yeye.

Kuza Wito Wako.

Tunapewa miito yetu kwa sababu, hata kama hatujui sababu toka mwanzo.

Nilishawahi mara moja kuitwa kwenye Urais wa Usaidizi wa Akina Mama wa kata ya vijana watu wazima waseja. Nilifurahia kuanza. Bali baada ya miezi michache, nilihisi kukata tamaa. Sikuweza kuona kukua kiroho katika wale niliokuwa nikiwahudumia. Juhudi zangu za kuwatembelea na kuwa karibu nao zilionekana kuanguka.

Jumapili moja, nilihisi kama nilikuwa nakosa kipawa cha kiroho ambacho humsaidia mtu kuwa mzuri katika kuhudumu. Sala yangu wakati wa sakramenti siku hiyo ilikuwa ni kuhisi uhakika kwamba nilikuwa na uwezo wa wito wangu. Nilihisi kuvutiwa kuomba baraka za kikuhani.

Nilikutana na askofu wangu, na alipoweka mikono yake kichwani mwangu, kitu cha kwanza alichosema kwangu ilikuwa ni, “Baba wa Mbinguni anafurahishwa na upendo unaoonyesha kwa wengine.

Roho alinifunika, na kuhisi uhakika kwamba Bwana alifurahishwa na juhudi zangu. Nilihisi kuwa na sehemu ya vipawa vilivyohitajika kutumikia kwa upendo. Nimekuwa nikipima kushindwa kwangu badala ya mafanikio yangu.

Wito wako ni nafasi kubwa sana kutafuta na kutumia vipawa vyako vya kiroho.

Unaweza Kuanza Sasa

Hatuhitaji kusubiri kuanza kugundua mazuri ndani yetu wenyewe.

Rais Dieter F.Uchtdorf, akiwa Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema:

“Wakati mwingine tunahisi kukata tamaa kwa sababu hatuko ‘zaidi’ wa kitu fulani —kiroho zaidi, kuheshimika, wenye akili, afya, tajiri, kirafiki, au wenye kuweza. …

“Nilijifunza maishani mwangu kwamba hatuhitaji kuwa ‘zaidi’ ya kitu chochote kuanza kuwa mtu ambaye Mungu angependa sisi tuwe.”5

Tunaweza kuanza kwa sala. Mwambie Baba wa Mbinguni jinsi unavyohisi sasa, na jinsi gani unapenda kuhisi kuhusu wewe mwenyewe. Haswa omba kipawa cha utambuzi kukusaidia kuona uzuri wako wa asili. Baadhi ya nyakati nzuri za maisha yangu yamekuja kutokana na kusema sala hizi. Naamini Baba wa Mbinguni ana shauku ya kutusaidia sisi kuona yale yote Anayoona.

Kwa sababu ya utambulisho wetu kama watoto wa Mungu, tuliokusudiwa kwa ajili ya ukuu (ona Mafundisho na Maagano 78:17). Kupitia kipawa cha utambuzi, tunatunaweza kuyajua hayo wenyewe.

Muhtasari

  1. Stephen L Richards, katika Douglas D. Holmes, “Ndani ya Mioyo Yetu,” Liahona, Mei 2020, 25–26.

  2. David A. Bednar, “Quick to Observe” (Brigham Young University devotional, Mei 10, 2005), 5, speeches.byu.edu; msisitizo umeongezwa.

  3. Larry R. Lawrence, “Nimepungukiwa Na Nini Tena?” Liahona, Nov. 2015, 35.

  4. Henry B. Eyring, “Daima Mkumbuke Yeye,” Ensign, Feb. 2018, 5.

  5. Dieter F. Uchtdorf, “Inafanya Kazi kwa Maajabu!” Liahona, Nov. 2015, 22-23.