2021
Fumbo la Kabaila: Fundisho katika Utiifu
Septemba/ Oktoba 2021


Njoo, Unifuate

Fumbo la Kabaila: Fundisho katika Utiifu

Mafundisho na Maagano 101

Mafundishi na Maagano 101:43–62 inatoa fumbo ambalo lilitolewa kuelezea kwa nini Watakatifu walifukuzwa kutoka Missouri.

Katika fumbo, mtumwa anaanza kujenga mnara lakini baadae anaamua kwamba “hakuna uhitaji” kwa ajili yake (Mafundisho na Maagano 101:49). Ila kwa sababu hawajengi mnara, hawana tahadhari wakati adui atakapovunja na kuharibu shamba la mizabibu.

Picha
illustrations from parable of the nobleman

Kabaila huagiza watumishi wake kulima shamba la mizabibu na kujenga ua kuzunguka miti na mnara ili kwamba mlinzi anaweza kuangalia juu ya nchi yote.

Watumishi hupanda shamba la mizabibu na kujenga kingo lakini wakaamua kutojenga mnara.

Adui asiyetarajiwa uharibu shamba la mzabibu.

Vielelezo na Ben Simonsen

Je, niliwahi kuhoji juu ya amri za Mungu?

Mmewahi, kama watumushi, kuwahi kushangaa ikiwa amri ilikuwa hakika ya lazima? Fumbo hili linatufundisha kwamba amri za Bwana hutulinda na kutusaidia sisi kuishi maisha ya furaha (ona pia Mosia 2:41; Mafundisho na Maagano 82:8–10).

Je, tunaweza kufanya nini kama hatuoni uhitaji wa amri?

  • Jifunze mada na usali katika Bwana kutusaidia “kuhisi kwamba ni sahihi.” (Mafundisho na Maagano 9:8).

  • Kumbuka nyakati katika siku za kale wakati utiifu ulipoleta baraka.1

  • Tenda katika imani, tukiamini kwamba tutaelewa “baada ya majaribu ya imani [yetu]” (Etheri 12:6).

Picha
article on parable of the nobleman

Muhtasari

  1. Ona Neil L. Andersen, “Kumbukumbu za Kuelekeza Kiroho,” Liahona, Mei 2020, 18–22.