2021
Kambi ya Sayuni—Kujiandaa Kumtumikia Bwana.
Septemba/ Oktoba 2021


Njoo, Unifuate

Kambi ya Sayuni—Kujiandaa Kumtumikia Bwana.

Mafundisho na Maagano 102–105

Picha
article on Zion’s Camp

Baada ya kundi la waumini wa Kanisa lijulikanalo kama Kambi ya Sayuni kutembea mamia ya maili kuwasaidia wenzao Watakatifu wa Siku za Mwisho, Bwana alimwambia Joseph Smith kutawanya kundi, ingawa hata hivyo walidhani hawakutimiza lengo lao. Kwa sababu hii, baadhi waliita Kambi ya Sayuni iliyoshindikana, bali wale walioshiriki walishuhudia kuwa uzoefu wao uliwaandaa kwa ajili ya utumishi wao kwa Bwana siku zijazo.

Wakati wa matembezi marefu, baadhi ya washiriki wa kambi walilalamika na nakusema dhidi ya Nabii Joseph, bali wengine walikuwa waaminifu kwake na walijifunza uvumilivu na utiifu.

  • Februari 1834: Joseph Smith alipokea ufunuo kutafuta angalau watu 100 kwenda Missouri na kusaidia Watakatifu kupata aridhi yao katika Kaunti ya Jackson.

  • Makundi 2 ambayo yalitumia njia tofauti yalikutana Juni.

  • Takriban wanaume 207 na, wanawake 25 na watoto walishiriki.

  • Walitembea kati ya maili 20–40 (kilomita 32 hadi 64) kwa siku.

  • Wengi walisafiri zaidi ya maili 900 (kilomita 1,450) kupitia majimbo 4.

  • Watakatifu 13 walifariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu kambini.

  • Mitume 8 kati ya 12 wa kwanza wa siku za mwisho walihudumu katika kambi hii.

  • Wote wa akidi ya Sabini wa siku za mwisho walikuwa washiriki wa kambi.

  • Juni 1834:Nabii Joseph alipokea ufunuo na kukubali matoleo ya washiriki wa kambi, kisha ikavunjwa.

Mjadala

Unafikiri inamaanisha nini kuikomboa Sayuni? (ona Mafundisho na Maagano 103:15).