2021
Jina la Kanisa na Kujenga Sayuni
Septemba/ Oktoba 2021


Kwa ajili ya Wazazi

Jina la Kanisa na Kujenga Sayuni

Wapendwa Wazazi,

Unaweza kutumia makala yafuatayo na picha zake kufungua majadiliano pamoja na familia yako na kuwasaidia kuelewa mada muhimu kama vile kutumia jina sahihi la Kanisa na kuijenga Sayuni.

Jina Sahihi la Kanisa

Someni kama familia baadhi ya hadithi kutoka kwenye makala ya Rais Eyring “Hivyo Ndivyo Kanisa Langu Litakavyoitwa,” kuanzia ukurasa wa 8. Fikiria kupitia upya hotuba ya Rais Nelson katika mada hii katika mkutano mkuu wa Oktoba 2018. Ni katika njia gani wewe na familia yako mmebarikiwa kadiri mlivyofanya juhudi kutumia jina sahihi la Kanisa—Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho?

Kujenga Sayuni

Waulize watoto wako wanacho fikiri Sayuni inamaanisha nini. Kisha tumia makala ya Mzee Gerrit W. Gong “Kuileta Sayuni” katika ukurasa wa 12 kuwasaidia kujifunza kujua Sayuni humaanisha nini hapo zamani na sasa. Fikiria kujadili njia ambazo familia yako inaweza kusaidia kujenga Sayuni nyumbani mwako na katika jamii yako.

Njoo, Unifuate Msaada wa Kujifunza

Ona ukurasa 26 kwa makala na mada tofauti katika Njoo, Unifuate kusaidia kujifunza kwako Mafundisho na Maagano kwa mwezi huu.