2021
Ninawezaje Kusaidia Kushinda Chuki?
Septemba/ Oktoba 2021


Ninawezaje Kusaidia Kushinda Chuki?

Zifuatazo ni njia sita za kuachana na chuki na kukuza heshima.

Picha
women sitting in circle enjoying sharing stories in group meeting

Je, Ninaweza kufanya Nini ili Kushinda Chuki?

1. Angalia ndani kwanza. Tunaweza kuweka lengo la kujiangalia ndani yetu na kuachana na “tabia na matendo ya chuki.”1

Rais Russell M. Nelson alisema, “Yeyote kati yetu ambaye ana chuki dhidi ya mbari nyingine anahitaji kutubu!”2

2. Tafuta kuelewa. Tenga muda wa kuwasikiliza wale waliopitia chuki. Hii inaweza kujumuisha vitabu, filamu na habari kuhusiana na mada.3

Darius Gray, Mmarekani mweusi na muumini maarufu na kiongozi wa Kanisa, alisema, “Ikiwa tungejitahidi kwa dhati kuwasikiliza wale tunaowaona kama ‘wengine’, na ikiwa fokasi yetu ya dhati ingekuwa kuwafanya washiriki maisha yao, historia zao, familia zao, matumaini yao, na machungu yao, sio tu tungepata uelewa zaidi, lakini jambo hili lingesonga mpaka kwenye kuponya vidonda vya ubaguzi wa rangi.”4

3. Paza Sauti. Kama utasikia mtu akishiriki wazo potofu au hasi kuhusu mbari, paza sauti kwa upendo na kwa usahihi.

Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alisema, “Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, lazima tufanye vizuri zaidi kusaidia kungo’a mizizi ya ubaguzi wa rangi.”5

Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha “tunaalikwa kuubadilisha ulimwengu kuwa bora, kutoka ndani kwenda nje, mtu mmoja, familia moja, kitongoji kimoja kwa wakati mmoja.”6

Naweza Kufanya Nini Ikiwa Nimepitia Unyanyapaa?

Picha
man in wheelchair communicates cheerfully with employees at the office

1. Samehe na tafuta rafiki. Tunapokuwa tumeumizwa kwa matendo ya wengine, tunaweza kufundisha na kusamehe na kutafuta kujenga uhusiano.

Wakati akihudumu kama Sabini wa Eneo, Mzee Fred A. ‘Tony” Parker alisema: “Nilipokuwa mhanga wa ubaguzi wa rangi, nimepata mafanikio kwa kukabiliana nao uso kwa uso, kumsamehe mtu huyo na kulizungumzia swala hilo. Ikiwa mtu anasema kitu kuumiza hisia zangu, ninahitaji kutafuta njia ya kumsaidia kuelewa kwa nini hilo linaumiza. Ni fursa sio tu ya kusamehe bali pia ya kujenga uhusiano ili kwamba mtu asimuangalie tu Tony Parker kama Mmarekani mweusi bali kama mtoto wa Mungu. Yesu alifundisha msamaha (ona Mathayo 18:21–35), na alitufunza kwamba tunapokosewa tulitatue na mtu huyo (ona Mathayo 18:15).”7

2. Jifunze masomo muhimu kutokana na uzoefu wa uchungu (ona Mafundisho na Maagano 122:7).

Mchungaji Amos C. Brown anasimulia hadithi kuhusu Howard Washington Thurman. Howard aliishi jirani na mwanamke aliyeinyanyasa familia yake kwa sababu walikuwa Weusi—kiasi cha kurusha mbolea ya kuku kutoka kwenye banda lake kwenda kwenye uwa wa Thurman.

Wakati mwanamke huyo alipougua, mama wa Howard alimpelekea supu na maua. Kwa shukrani, yule mwanamke aliuliza sehemu yalipotoka yale maua. Mke wa Thurman alisema, “Wakati uliporusha mbolea ya kuku, Mungu alikuwa anauandaa udongo.”

“Hilo ndilo tunatakiwa kufanya katikati ya uovu,” Mchungaji Brown alisema. “Chukua mbolea lakini kuwa na imani kwa Mungu ya kuitumia mbolea hiyo kupanda bustani ya maua.”8

3. Mgeukie Kristo kwa ajili ya uponyaji na mwongozo. Kumwamini Mwokozi kwa machungu yako na kumfuata yeye kunaweza kuleta amani.

Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba kwa kuongezea katika kutukomboa kutoka dhambini kwa kutimiza matakwa ambayo haki inayo juu yetu, Yesu Kristo “pia alitimiza deni tunalodaiwa na haki kwa kuponya na kulipia kwa mateso yoyote tunayovumilia.”9

Mwokozi aliweka mfano mkamilifu wa sisi kufuata. Alitufundisha jinsi ya kufanya tunapokosewa (ona Mathayo 18:15), tunapoteswa (ona Mathayo 5:38–48), na kuhukumiwa kifo pasipo haki (ona Luka 23:34).

Muhtasari

  1. General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 38.6.14, ChurchofJesusChrist.org.

  2. Russell M. Nelson, katika “President Nelson Shares Social Post about Racism and Calls for Respect for Human Dignity,” Newsroom, June 1, 2020, newsroom.ChurchofJesusChrist.org.

  3. Ona “Tafuta Taarifa kutoka kwenye Vyanzo vya Kuaminika,” General Handbook, 38.8.45.

  4. Darius Gray, “Healing the Wounds of Racism,” Apr. 5, 2018, blog.ChurchofJesusChrist.org.

  5. Dallin H. Oaks, “Wapendeni Adui Zenu,” Liahona, Nov. 2020, 28.

  6. Gerrit W. Gong, “Mataifa Yote, Kabila na Lugha,” Liahona, Nov. 2020, 38.

  7. Fred A. “Tony” Parker, Mwokozi Anaponya Maumivu Yetu,” Ensign, Juni 2018, 44–45.

  8. “Sisi ni Familia: Mjadala juu ya Kushinda Chuki na Mzee Jack N. Gerard na Mchungaji Amos C. Brown,” Liahona, Sept. 2021, toleo la kidijitali.

  9. D. Todd Christofferson, “Ukombozi,” Liahona, Mei 2013, 110.