Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 84


Sehemu ya 84

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, tarehe 22 na 23 Septemba 22 na 23, 1832. Katika kipindi cha mwezi wa Septemba, wazee walikuwa wamekwisha anza kurejea kutoka katika kazi zao za umisionari katika nchi za mashariki na kutoa ripoti ya kazi zao. Ilikuwa wakati walipokuwa pamoja katika majira haya ya shangwe kwamba mawasiliano haya yafuatayo yalipokelewa. Nabii aliyaita kama ufunuo juu ya ukuhani.

1–5, Yerusalemu Mpya na hekalu vitajengwa katika Missouri; 6–17, Safu ya ukuhani yatolewa kutoka Musa mpaka Adamu; 18–25, Ukuhani mkuu hushikilia ufunguo wa ufahamu wa Mungu; 26–32, Ukuhani mdogo hushikilia ufunguo wa kuhudumiwa na malaika na wa injili ya matayarisho; 33–44, Wanaume hupata uzima wa milele kwa njia ya kiapo na agano la ukuhani; 45–53, Roho wa Kristo huwaangaza watu, na dunia hukaa katika dhambi; 54–61, Watakatifu ni lazima washuhudie mambo yale waliyoyapokea; 62–76, Wao wataihubiri injili, na ishara zitawafuata; 77–91, Wazee watakwenda pasipo mfuko wala mkoba, na Bwana atawatimizia mahitaji yao; 92–97, Magonjwa na laana zinawasubiri wale wanaoikataa injili; 98–102, Wimbo mpya wa ukombozi wa Sayuni unatolewa; 103–110, Kila mtu na asimame katika ofisi yake mwenyewe na kufanya kazi katika wito wake mwenyewe; 111–120, Watumishi wa Bwana watahubiri chukizo la uharibifu la siku za mwisho.

1 Ufunuo wa Yesu Kristo kwa mtumishi wake Joseph Smith, Mdogo, na wazee sita, kama vile walivyounganisha mioyo yao na akupaza sauti zao juu.

2 Ndiyo, neno la Bwana kuhusu kanisa lake, lililoanzishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili ya aurejesho wa watu wake, kama alivyonena kwa vinywa vya bmanabii wake, na kwa ajili ya kuwakusanya cwatakatifu wake ili wasimame juu ya dMlima Sayuni, ambao utakuwa mji wa eYerusalemu Mpya.

3 Mji ambao utajengwa, kuanzia sehemu ya kiwanja cha ahekalu, mahali ambapo pameteuliwa kwa kidole cha Bwana, katika mipaka ya Jimbo la Missouri, na kuwekwa wakfu kwa mkono wa Joseph Smith, Mdogo, na wengine ambao Bwana alipendezwa nao sana.

4 Amini hili ndilo neno la Bwana, kwamba mji wa aYerusalemu Mpya utajengwa kwa kukusanyika kwa watakatifu, kuanzia mahali hapa, hata mahali pa bhekalu, hekalu ambalo litainuliwa katika kizazi hiki

5 Kwani amini kizazi hiki chote hakitapita hadi nyumba itakapojengwa kwa Bwana, na wingu litatulia juu yake, wingu ambalo litakuwa hata autukufu wa Bwana, ambalo litaijaza nyumba.

6 Na wana wa Musa, kulingana na Ukuhani Mtakatifu ambao aliupokea chini ya amkono wa baba mkwe wake, bYethro;

7 Na Yethro aliupokea chini ya mkono wa Kalebu;

8 Na Kalebu aliupokea chini ya mkono wa Elihu;

9 Na Elihu chini ya mkono wa Yeremia;

10 Na Yeremia chini ya mkono wa Gadi;

11 Na Gadi chini ya mkono wa Isaya;

12 Na Isaya aliupokea chini ya mkono wa Mungu.

13 Isaya pia aliishi katika siku za Ibrahimu, na akabarikiwa naye,

14 aIbrahimu ambaye aliupokea ukuhani kutoka kwa bMelkizedeki, ambaye aliupokea kupitia safu ya baba zake, hata mpaka cNuhu;

15 Na kutoka Nuhu hadi aHenoko, kupitia safu ya baba zao;

16 Na kutoka Henoko mpaka aHabili, aliyeuawa kwa bnjama za kaka yake, caliyeupokea ukuhani kwa amri za Mungu, kwa mkono wa baba yake dAdamu, aliyekuwa mwanadamu wa kwanza—

17 aUkuhani ambao unaendelea katika kanisa la Mungu katika vizazi vyote, nao hauna mwanzo wa siku au mwisho wa miaka.

18 Na Bwana pia alithibitisha aukuhani pia juu ya bHaruni na uzao wake, kupitia vizazi vyake vyote, ukuhani ambao pia hudumu na ckukaa milele pamoja na ukuhani ambao ni wa mfano mtakatifu zaidi wa Mungu.

19 Na ukuhani huu mkuu huihudumia injili na hushikilia ufunguo wa asiri za ufalme, hata ufunguo wa bufahamu wa Mungu.

20 Kwa hiyo, katika aibada hizo, nguvu za uchamungu hujidhihirisha

21 Na pasipo ibada hizo, na amamlaka ya ukuhani, nguvu za uchamungu haziwezi kujidhihirisha kwa mwanadamu katika mwili;

22 Kwani pasipo hizi hakuna amwanadamu anayeweza kuuona uso wa Mungu, hata Baba, na kuishi.

23 Sasa aMusa alilifundisha hili kwa uwazi kabisa kwa wana wa Israeli nyikani, na alitafuta kwa bidii kubwa bkuwatakasa watu wake ili waweze ckuuona uso wa Mungu;

24 Lakini awaliishupaza mioyo yao na kushindwa kustahimili uwepo wake; kwa sababu hii, Bwana katika bghadhabu yake, kwani hasira yake iliwaka dhidi yao, akaapa kuwa chawataingia rahani mwake wakati wakiwa nyikani, raha ambayo ni utimilifu wa utukufu wake.

25 Kwa hiyo, alimchukua aMusa kutoka katikati yao, na bUkuhani Mtakatifu pia;

26 Na aukuhani mdogo uliendelea, ukuhani ambao hushikilia bufunguo wa ckuhudumiwa na malaika na wa injili ya matayarisho;

27 Injili hii ambayo ni injili ya atoba na ya bubatizo, na condoleo la dhambi, na dsheria ya amri ya ekimwili, ambao Bwana katika ghadhabu yake aliifanya iendelee pamoja na nyumba ya Haruni miongoni mwa wana wa Israeli hadi fYohana, ambaye Mungu alimwinua, akiwa gamejazwa Roho Mtakatifu tokea tumboni mwa mama yake.

28 Kwani yeye alibatizwa wakati akiwa bado mtoto, na alitawazwa na malaika wa Mungu wakati akiwa na umri wa siku nane katika uwezo huu, kuupindua ufalme wa Wayahudi, na kuyanyoosha mapito ya Bwana mbele ya uso wa watu wake, kwa akuwatayarisha kwa ujio wa Bwana, ambaye mikononi mwake umetolewa buwezo wote.

29 Na tena, ofisi za mzee na askofu, ni aviambatanisho muhimu vya ukuhani mkuu.

30 Na tena, ofisi za mwalimu na shemasi ni viambatanisho muhimu vya ukuhani mdogo, ukuhani ambao ulitolewa kwa Haruni na wanawe.

31 Kwa hiyo, kama nilivyosema kuhusu wana wa Musa—kwani wana wa Musa na pia wana wa Haruni watatoa amatoleo na dhabihu yaliyokubalika katika nyumba ya Bwana, nyumba ambayo itajengwa kwa ajili ya Bwana katika kizazi hiki, juu ya beneo lilowekwa wakfu kama nilivyolichagua—

32 Na wana wa Musa na wa Haruni watajazwa na autukufu wa Bwana, juu ya bMlima Sayuni katika nyumba ya Bwana, wana ambao ni ninyi; na pia wengi ambao nimewaita na kuwatuma kulijenga ckanisa langu.

33 Kwani yeyote aaliye mwaminifu katika kupata bkuhani hizi mbili ambazo nimezinena, na kutukuza wito wake, chutakaswa na Roho kwa kufanywa upya miili yao.

34 Wanakuwa wana wa Musa na Haruni na auzao wa bIbrahimu, na kanisa na ufalme, na cwateule wa Mungu.

35 Na pia wale wote waupokeao ukuhani huu wananipokea Mimi, asema Bwana;

36 Kwani yule awapokeaye watumishi wangu aanipokea Mimi;

37 Na yule aanipokeaye mimi ampokea Baba yangu;

38 Na yule ambaye ampokea Baba yangu aupokea ufalme wa Baba yangu; kwa hiyo yale ayote Baba yangu aliyonayo atapewa.

39 Na hii ni kulingana na akiapo na agano lihusianalo na ukuhani.

40 Kwa hiyo, wale wote waupokeao ukuhani, hupokea kiapo hiki na agano hili la Baba yangu, ambalo haliwezi kuvunjwa, wala kuondolewa.

41 Lakini yeyote aavunjaye agano hili baada ya kulipokea, na kuligeuka kabisa, bhatapata msamaha wa dhambi katika ulimwengu huu wala ulimwengu ujao.

42 Na ole wao wale wote wasiokuja katika ukuhani huu ambao ninyi mmeupokea, ambao sasa ninauthibitisha juu yenu ninyi mlioko hapa leo, kwa sauti yangu mwenyewe kutoka mbinguni; na hata nimewapa majeshi ya mbinguni na amalaika wangu wajibu juu yenu.

43 Na sasa mimi ninatoa kwenu ninyi amri ya kuwa waangalifu juu yenu wenyewe, ili kufanya bidii ya ausikivu kwa maneno ya uzima wa milele.

44 Kwani amtaishi kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.

45 Kwa kuwa aneno la Bwana ni ukweli, na lolote lililo bkweli ni nuru, na lolote lililo nuru ni Roho, hata Roho wa Yesu Kristo.

46 Na Roho hutoa anuru kwa bkila mtu ajaye katika ulimwengu; na Roho humwangazia kila mtu kote ulimwenguni, yule aisikilizaye sauti ya Roho.

47 Na kila mtu aisikilizaye sauti ya Roho huja kwa Mungu, hata Baba.

48 Na Baba ahumfundisha bagano ambalo amelifanya upya na kulithibitisha juu yenu ninyi, ambalo limethibitishwa juu yenu kwa faida yenu, na siyo kwa faida yenu peke yake, bali kwa faida ya ulimwengu wote.

49 Na adunia yote hukaa katika dhambi, na kuugulia bgizani na chini ya utumwa wa dhambi.

50 Na kwa hili muweze kujua wao wako chini ya autumwa wa bdhambi, kwa sababu hawaji kwangu.

51 Kwani yeyote asiyekuja kwangu yu chini ya utumwa wa dhambi.

52 Na yeyote asiye ipokea sauti yangu hajaizoea asauti yangu, na huyo siyo wangu.

53 Na kwa hili muweze kuwatambua kati ya wema na wabaya, na ya kwamba aulimwengu wote bunaugulia cdhambini na gizani hata sasa.

54 Na akili zenu katika wakati uliopita zilitiwa giza kwa sababu ya akutokuamini, na kwa sababu ya kuyachukulia bila uzito mambo mliyoyapokea—

55 aKiburi na kutokuamini ambako kumelileta kanisa lote chini ya hatia.

56 Na hatia hii i juu ya watoto wa Sayuni, hata wote.

57 Na watabakia chini ya hatia hii hadi watubu na kukumbuka aagano jipya, hata bKitabu cha Mormoni na amri za czamani ambazo niliwapa, siyo tu kwa kusema, bali kwa dkuzitenda kulingana na lile nililoliandika—

58 Ili waweze kuzaa matunda kwa ajili ya ufalme wa Baba yao; vinginevyo hapo hubaki mateso na hukumu kumwagwa juu ya watoto wa Sayuni.

59 Je, kwani watoto wa ufalme wataichafua nchi takatifu? Amini, ninawaambia, Hapana.

60 Amini, amini, ninawaambia ambao sasa mnayasikia amaneno yangu, ambayo ni sauti yangu, mmebarikiwa ninyi ilimradi mnayapokea mambo haya;

61 Kwani anitawasamehe dhambi zenu kwa amri hii—kwamba ninyi muendelee kuwa thabiti katika mawazo yenu katika btaadhima na roho ya sala, katika kutoa ushuhuda kwa walimwengu wote kwa yale mambo yote ambayo yamejulishwa kwenu.

62 Kwa hiyo, aenendeni ulimwenguni kote; na mahali popote ambako ninyi hamwezi kwenda mtautuma, ili ushuhuda uweze kwenda kutoka kwenu ninyi hadi ulimwenguni kote kwa kila kiumbe.

63 Na kama vile nilivyosema kwa amitume wangu, vivyo hivyo ninawaambia, kuwa ninyi ni mitume wangu, hata makuhani wakuu wa Mungu; ninyi ndiyo wale ambao baba bamenipa; ninyi ni cmarafiki zangu;

64 Kwa hiyo, kama vile nilivyosema kwa mitume wangu ninawaambia ninyi tena, kuwa kila amtu bayaaminiye maneno yenu, na kubatizwa kwa maji kwa ajili ya condoleo la dhambi, atampokea dRoho Mtakatifu.

65 Na ishara hizi azitawafuata hao wanaoamini—

66 Katika jina langu watafanya amiujiza mingi;

67 Katika ajina langu watawafukuza pepo wabaya;

68 Katika jina langu awatawaponya wagonjwa;

69 Katika jina langu watafungua macho ya vipofu, na kuzibua masikio ya viziwi;

70 Na ulimi wake aliye bubu utasema;

71 Na kama mtu yeyote atawawekea asumu haitawadhuru;

72 Na sumu ya nyoka haitakuwa na uwezo wa kuwadhuru.

73 Lakini amri ninaitoa kwao, kwamba awasijivune wenyewe kwa mambo haya, wala kuyanena mbele za walimwengu; kwani mambo haya yametolewa kwenu kwa faida na wokovu wenu.

74 Amini, amini, ninawaambia, wale wasioamini juu ya maneno yenu, na ahawajabatizwa katika maji katika jina langu, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao, ili waweze kumpokea Roho Mtakatifu, bwatahukumiwa, na hawatakuja katika ufalme wa Baba yangu mahali ambapo Baba na Mimi tupo.

75 Na ufunuo huu kwenu, na amri hii, vinaanza kutumika saa hii hii juu ya ulimwengu wote, na injili hii ni kwa wale wote ambao hawajaipokea.

76 Lakini, amini ninawaambia wale wote ambao kwao ufalme huu umetolewa—kutoka kwenu lazima ihubiriwe kwao, ili waweze kutubu matendo yao maovu ya zamani; kwani watakemewa kwa ajili ya mioyo yao miovu ya kutokuamini, na ndugu zenu katika Sayuni kwa uasi wao dhidi yenu wakati ule nilipowatuma.

77 Na tena ninawaambia, marafiki zangu, kwani kuanzia sasa nitawaita ninyi marafiki, ni muhimu kwamba niwape amri hii, ili muweze kuwa kama marafiki zangu katika siku zile wakati nilipokuwa pamoja nao, wakisafiri kuhubiri injili kwa uwezo wangu;

78 Kwani sikuwaruhusu kwenda na amfuko au mkoba, wala kanzu mbili.

79 Tazama, ninawatuma ninyi kwenda kuuthibitisha ulimwengu, na mfanyakazi anastahili aujira wake.

80 Na mtu yeyote atakaye kwenda na akuhubiri binjili hii ya ufalme, na asishindwe kuendelea kwa uaminifu katika mambo yote, hatachoka akilini, wala kutiwa giza, wala mwilini, mkononi, au viungo; na hautapotea hata cunywele mmoja wa kichwa chake. Na hawatakwenda na njaa, wala kiu.

81 Kwa hiyo, amsisumbukie juu ya kesho, kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, au mtavaa nini.

82 Kwani, fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo, hayafanyi kazi, wala hayasokoti; na falme za ulimwengu, katika utukufu wao wote, hazijavikwa vizuri kama mojawapo ya haya.

83 Kwani aBaba yenu, aliye mbinguni, bajua kwamba mnayo haja ya mambo hayo yote.

84 Kwa hiyo, kesho aijisumbukie yenyewe.

85 Wala msiwaze kabla anini cha kusema; bali byahifadhini katika akili zenu daima maneno ya uzima, nanyi cmtapewa saa ile ile mtakayosema sehemu ile ambayo itakayokusudiwa kwa kila mtu.

86 Kwa hiyo, pasiwepo mtu yeyote miongoni mwenu, kwani sheria hii ni kwa awaaminifu wote walioitwa na Mungu katika kanisa kwa huduma, kutoka sasa kuchukua mfuko au mkoba, yule aendaye kuitangaza injili hii ya ufalme.

87 Tazama, aninawatuma ninyi kuwakemea walimwengu kwa sababu ya matendo yao yote yasiyo ya haki, na kuwafundisha juu ya hukumu ambayo itakuja.

88 Na yeyote aawapokeaye ninyi, hapo nitakuwepo pia, kwani nitakwenda mbele ya uso wenu. Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na bmalaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu.

89 Yeyote awapokeaye ninyi ananipokea Mimi; naye atawalisha, na kuwavika, na kuwapa fedha.

90 Na yule awalishaye, au kuwavika, au kuwapa fedha, kwa vyovyote ahatapoteza kamwe thawabu yake.

91 Na yule asiyewafanyia mambo haya siyo mwanafunzi wangu; kwa njia hii mtaweza kuwajua awanafunzi wangu.

92 Mtu asiyewapokea, ondokeni kwake ninyi wenyewe, na aisafisheni miguu yenu hata kwa maji, maji safi, iwe katika joto au baridi, na toeni ushuhuda wake kwa Baba yenu aliye mbinguni, na msirudi tena kwa mtu huyo.

93 Na katika kijiji chochote au mji muingiao, fanyeni vivyo hivyo.

94 Hata hivyo, tafuteni kwa bidii na msiache; na ole wake nyumba ile, au kijiji kile au mji ule uwakataao ninyi, au maneno yenu, au ushuhuda wenu juu yangu.

95 Ole, nasema tena, kwa nyumba ile, au kijiji kile au mji ule uwakataao ninyi, au maneno yenu, au ushuhuda wenu juu yangu Mimi;

96 Kwani, Mimi, aMwenyezi, nimeweka mikono yangu juu ya mataifa, bkuwaadhibu kwa cuovu wao.

97 Na magonjwa yataenea, na hayataondolewa duniani hadi nitakapomaliza kazi yangu, ambayo aitafupishwa kwa haki—

98 Hadi wote watanijua, wanaobaki, hata kuanzia mdogo wao hata mkubwa wao, nao watajawa na kumjua Bwana, na wataona ajicho kwa jicho, na watapaza sauti zao, na kwa sauti bwataimba pamoja wimbo huu mpya, wakisema:

99 Bwana ameirejesha tena Sayuni;Bwana aamewakomboa watu wake, bIsraeli,Kulingana na cuchaguzi wa dneema,Ambao ulitimizwa kwa imaniNa eagano la Baba zao.

100 Bwana amewakomboa watu wake;Na Shetani aamefungwa na muda umekwisha.Bwana amevijumlisha vitu vyote katika bkimoja.Bwana ameishusha cSayuni kutoka juu.Bwana dameiinua Sayuni kutoka chini.

101 aDunia imepata utungu na kuzaa uwezo wake;Na kweli imeenea katika tumbo lake;Na mbingu zimetabasamu juu yake;Naye amevikwa kwa butukufu wa Mungu wake;Kwani yeye husimama katikati ya watu wake.

102 Utukufu, na heshima, na uwezo, na nguvu,Ziwe kwa Mungu wetu; kwa kuwa amejaa arehema,Haki, neema na kweli, na bamani,Milele na milele. Amina.

103 Na tena, amini, amini, ninawaambia, ni muhimu kwamba kila mtu anayekwenda kuihubiri injili yangu isiyo na mwisho, kwamba ilimradi wao wanazo familia, na wanapokea fedha kama zawadi, yawapasa wazitume kwao au wazitumie kwa manufaa yao, kama vile Bwana atakavyowaelekeza, kwa kuwa hivyo ndivyo nionavyo kuwa ni vema.

104 Na kwa wale wote wasio na familia, ambao wanapokea afedha, na wazitume kwa askofu katika Sayuni, au kwa askofu katika Ohio, ili ziweze kuwekwa wakfu kwa ajili ya kuleta mafunuo na kupiga chapa, na kwa ustawishaji wa Sayuni.

105 Na kama mtu yeyote atatoa kanzu kwa mtu yeyote kati yenu, au suti, achukue ile ya zamani na kumpa amaskini, na nenda zako ukifurahia.

106 Na kama mtu yeyote miongoni mwenu akiwa imara katika Roho, na aamchukue yule aliye dhaifu pamoja naye, ili aweze kuelekezwa katika bunyenyekevu kamili, ili naye aweze kuwa imara pia.

107 Kwa hiyo, wachukueni pamoja nanyi wale waliotawazwa katika aukuhani mdogo, na kuwatuma mbele yenu kuweka ahadi, na kuitengeneza njia, na kutimiza miadi ambayo ninyi wenyewe hamwezi kuitimiza.

108 Tazama, hii ndiyo njia ambayo mitume wangu, katika siku za zamani, walinijengea kanisa langu.

109 Kwa hiyo, kila mtu na asimame katika nafasi yake mwenyewe, na kutenda kazi katika wito wake mwenyewe; na wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu sina haja na wewe; kwani pasipo miguu mwili wawezaje kusimama?

110 Pia mwili unahitaji kila akiungo, ili wote uweze kujengwa kwa pamoja, ili muundo uweze kubaki mkamilifu.

111 Na tazama, amakuhani wakuu wanapaswa kusafiri, na pia wazee, na pia bmakuhani wadogo; lakini cmashemasi na dwalimu yapasa wateuliwe ekuliangalia kanisa, kuwa wahudumu wa kudumu kwa kanisa.

112 Na askofu, Newel K. Whitney, pia anapaswa kusafiri maeneo ya jirani na miongoni mwa makanisa yote, akiwatafuta maskini na akuhudumia mahitaji yao kwa bkuwanyenyekeza matajiri na wenye majivuno.

113 Yampasa pia kuajiri awakala atakayekuwa akiwajibika na kufanya shughuli zake za kawaida kama yeye atakavyoelekeza.

114 Hata hivyo, askofu na aende katika mji wa New York, pia katika mji wa Albany, na pia mji wa Boston, na kuwaonya watu wa miji hiyo kwa sauti ya injili, kwa sauti kubwa, juu ya amaangamizo, na maangamizo makamilifu ambayo yanawasubiri ikiwa wanayakataa mambo haya.

115 Kwani ikiwa wanayakataa mambo haya saa ya hukumu yao i karibu, na nyumba yao aitaachwa.

116 Na aanitegemee mimi na wala bhatashindwa; na hata cunywele mmoja wa kichwa chake hautapotea.

117 Na amini ninawaambia, watumishi mliosalia, nendeni kadiri hali zenu zitakavyowaruhusu, katika miito yenu mbalimbali, kwenye miji mikuu na vijiji, mkiukemea ulimwengu katika haki juu ya matendo yao yote yasiyo ya haki na yasiyo ya uchamungu, mkielezea vizuri na kwa kueleweka chukizo la uharibifu katika siku za mwisho.

118 Kwani, pamoja nanyi asema Bwana Mwenyezi, anitaziharibu falme zao; siyo tu bnitaitikisa dunia, bali mbingu ya nyota itatikisika.

119 Kwani Mimi, Bwana, nimeunyosha mkono wangu ili kuzitakasa nguvu za mbinguni; hamwezi kuona hili sasa, bado kipindi kifupi nanyi mtaona, na kujua kuwa Mimi ndiye, na kwamba anitakuja na bkutawala pamoja na watu wangu.

120 Mimi ni aAlfa na Omega, mwanzo na mwisho. Amina.