Misaada ya Kujifunza
Henoko


Henoko

Nabii aliyewaongoza watu wa mji wa Sayuni. Huduma yake inaongelewa kote katika Agano la Kale na Lulu ya Thamani Kuu. Yeye alikuwa patriaki wa saba baada ya Adamu. Alikuwa mwana wa Yaredi na baba wa Methusela (Mwa. 5:18–24; Lk. 3:37).

Henoko alikuwa mtu maarufu na alikuwa na huduma iliyokuwa muhimu zaidi kuliko historia fupi inayoonyeshwa katika Biblia juu yake. Biblia inaandika kwamba yeye alihamishwa (Ebr. 11:5) lakini haitoi maelezo juu ya huduma yake. Yuda 1:14 inayo nukuu za unabii alioufanya. Ufunuo wa siku za mwisho unaelezea zaidi juu ya Henoko, hususani juu ya mahubiri yake, mji wake uliitwa Sayuni, maono yake, na unabii wake (M&M 107:48–57; Musa 6–7). Sayuni ulitwaliwa mbinguni kwa sababu ya haki ya wale walioishi ndani yake (Musa 7:69).