Misaada ya Kujifunza
Agano


Agano

Makubaliano kati ya Mungu na mwanadamu, lakini hawatendi kama walio sawa katika makubaliano hayo. Mungu hutoa masharti ya agano, na wanadamu hukubali kutenda yale Yeye aliyowaagiza kuyafanya. Ndipo Mungu huwaahidi wanadamu baraka fulani kwa utiifu wao.

Kanuni na ibada hupokelewa kwa agano. Waumini wa Kanisa wafanyao maagano ya namna hiyo huahidi kuyaheshimu. Kwa mfano, waumini huagana na Bwana wakati wa ubatizo na kurudia agano hilo kwa kupokea sakramenti. Hufanya maagano mengine zaidi katika hekalu. Watu wa Bwana ni watu wa agano nao hubarikiwa sana kadiri wanavyoshika maagano yao na Bwana.