2021
Mafunzo (na Chakula) kutoka kwenye Shamba la Kata
Machi 2021


SAUTI ZA WAUMINI

Mafunzo (na Chakula) kutoka kwenye Shamba la Kata

Wakati watu wanapofanikiwa, wanasema, “kutoka kwenye nyasi mpaka kwenye neema” lakini katika muktadha wa shamba la kata, kirai “kutoka kwenye uchafu mpaka kwenye ladha” kingefaa zaidi kutumika.

Viongozi wa Kanisa wametushauri, kama waumini, kulima bustani katika nyumba zetu. Hivi karibuni, waumini kutoka Kata ya Mountain View huko Nairobi, Kenya walitii ushauri huo—na kufuatia jukumu kutoka kwa askofu wao—walifanya kazi kwa bidii kutengeneza shamba la kata (neno ‘shamba’ linamaansha ‘bustani’ katika Kiswahili). Waumini wa kata waliungana na kutumia maarifa yao katika kubadilisha vichaka vya miiba na nyasi kuwa mavuno mengi.

Kaka Michael Bahati alisema kwamba siku zote amekuwa akitaka kutumia ujuzi wake wa kilimo kwenye shamba, akisema kwamba kwa kiasi anachoweza kukumbuka shamba limeachwa kwa muda mrefu. Kaka Bahati alihakikisha kwamba alitenga muda wa kutosha ili kulima, kuweka mbolea, kupandikiza vichipukizi na kupogoa. Ingemsikitisha Bahati kama angepoteza mavuno, ambayo hayakuwa tu kwa ajili yake mwenyewe lakini yalitunzwa kwa ajili ya manufaa ya waumini wote wa kata.

Maneno kutoka Yakobo 5:62, “Kwa hivyo, hebu twende na tutumike kwa nguvu zetu . . .” yanaelezea pia juhudi za Askofu Musaka. Aliendesha gari kwenda kanisani kila wikiendi, alikunja mikono ya shati lake na kufanya kazi kwa bidii. Aliwajua waumini wake, alielewa mahitaji yao, na kufanya kazi pamoja nao. Kwa kuwa askofu pia ni rais wa akidi ya makuhani, alihakikisha kwamba makuhani hawakuachwa nyuma, na aliwaalika kufanya kazi.

Kaka Bonabol alikuwa miongoni mwa wale walioitikia wito wa askofu. Alilibeba jukumu kama lake, ili kuhakikisha kwamba kuna chakula cha kutosha kwa ajili ya waumini. Aliliona kama jukumu lake la ukuhani, na alilitimiza kwa heshima.

Dada Omondi alikuwa na tabia ya kufanya mazoezi kila asubuhi, akikimbia kutoka nyumbani kwake mpaka Uthiru. Kisha alifikiria kwamba kuna kitu cha ziada angeweza kufanya. Aliwasiliana na Kaka Vidonyi, ambaye alimtaarifu kwamba kulikuwa na kazi ya kufanya shambani. Hivyo ndivyo mbio zake za asubuhi zilivyobadilishwa kwa kazi ya shamba.

Waumini wa kata ambao hapo awali walikuwa wakifanya kazi hapo walikuwa na ujuzi kidogo katika kupanda, hivyo Dada Omondi aliwafundisha jinsi ya kulima na kupanda. Alielezea uzoefu wake hivi: “Nilikuwa na shaka kama karanga zitaota, lakini ziliota na japo viazi vilipandwa katika mfumo usio sahihi, viliweka mizizi.” Jukumu kuu la Dada Omondi lilikuwa kumwagilizia mimea na alijifunza jukumu lake na kutenda katika ofisi yake aliyoteuliwa kwa utiifu mkuu.

Kadiri ilivyokuwa fursa ya kujifunza kwa Kaka Omondi, yeye pia alitumia fursa na kuwafundisha wengine. Udongo wa kanisani haukuwa mgeni kwake na alielewa kipi kitachanua vyema katika shamba.

Dada Mahindi alikuwa na wasiwasi juu ya ugonjwa wa binti yake lakini aliona ni bora kama ataondoa akili yake kwenye hilo. Alihisi kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii kwenye shamba, mambo yangeimarika—na yaliimarika. Alipata faraja na amani wakati binti yake akipata nafuu.

Askofu Mukasa alihakikisha inawezekana kwa waumini kumwagilia mimea. Alihakikisha kuna mabomba ya kutosha ya kutumia wakati wakisubiria kinyunyiza maji. Alisema, “Kama mimea inavyohitaji maji ili irutubishwe, waumini pia wanahitaji virutubisho kutoka kwenye maandiko matakatifu.” Mimea haikuweza kukaa siku moja bila maji, kama ambavyo waumini hawapaswi kupoteza siku moja bila kujifunza maandiko yao.

Wamisionari pia walifanikiwa kuwaleta wachunguzi wa kanisa ili kufanya kazi katika shamba. Ni fursa iliyoje wachunguzi hao wa kanisa walipewa ya kupokea injili ya urejesho na wakati huo huo walipokea chakula kutoka kwenye bustani ambayo waliifanyia kazi.

Mwishowe, siku ilikuja ambapo thawabu zilikuwa zikionekana dhahiri na kwa wingi. Kazi kubwa ya waumini wa kata ya Mountain View ilijidhihirisha yenyewe. Kulikuwa na wingi wa chakula, kuanzia ndizi mpaka kwenye mboga kwenye maharage na wako karibu kuvuna mahindi. Ilikuwa dhahiri kwamba lengo la waumini halikuwa kwa ajili ya majigambo ya papo hapo. Walielewa kwamba katika mavuno yote, baadhi ya baraka haziji mpaka baadae, hivyo walichagua kuwa na subira kwenye viazi vitamu na mihogo.

Kadiri nilivyofanya kazi kwenye shamba na kuliona likipiga hatua, niliona badiliko kwangu mwenyewe. Kama mmea uliotunzwa vizuri na Bwana ulizaa jinsi Yeye alivyotamani, je naweza kumhusisha Bwana na kumruhusu Yeye kuniongoza kufikia kiwango changu na kuishi ndani ya fursa zangu? Funzo langu kutoka kwenye shamba linajibu, “Ndio!”

Marc Otieno ni Kiongozi wa Wamisionari wa Kata katika Kata ya Mountain View, Kigingi cha Nairobi West.