2022
Misheni yako na Fumbo la Urithi Uliofichwa Ardhini
Machi 2022


UJUMBE WA URAIS WA ENEO

Misheni yako na Fumbo la Urithi Uliofichwa Ardhini

Watoto wa mtu tajiri katika fumbo waligundua kwamba muda unafika wakati ambapo unalazimika kutegemea ushuhuda wako mwenyewe wa kweli za Maisha—jambo ambalo huja kutokana na juhudi binafsi.

Hadithi iliyosisimua fikra zangu changa katika miaka ya ujana wangu ni ile ya mtu tajiri aliyemiliki bustani kubwa la matunda. Alikuwa na shida moja tu. Watoto wake walikua wakubwa katika wakati ambao bustani yake ya matunda tayari ilikuwa imemfanya kuwa tajiri. Alikuwa na watumishi wengi na hivyo watoto hawakuhitaji kufanya kazi yoyote ngumu. Aligundua kwamba watoto hawakuvutiwa na bustani ya matunda. Walichukulia kufanya kazi bustanini kama kazi ya watumishi. Ilikuwa kazi ngumu na isiyo na mvuto kwao. Kwa lengo la makala hii, nitarejelea hadithi kama fumbo la urithi uliofichwa ardhini.

Mtu tajiri alikuwa na wasiwasi kuhusu magumu ambayo watoto wake wangekabiliana nayo baada ya kifo chake ikiwa wangeendelea katika mtazamo ule. Hivyo siku moja, aliwaita pamoja na kuwaambia kwamba ameandika urithi ambao ndani yake angempa kila mmoja wao sehemu ya hazina alizokuwa amekusanya kwa ajili ya urithi wao. Alikuwa amefunga urithi na wangeweza tu kuufungua baada ya kifo chake. Hivyo kulikuwa na matazamio mengi kati ya watoto baada ya baba yao kufariki. Kila mmoja alitazamia kuchukua gawio lake la urithi na kuendelea kuishi maisha yaliyojawa urahisi na faraja yenye mengi ya kufurahia.

Siku ya kugundua kile kilichokua kwenye urithi hatimaye iliwadia. Kwenye urithi, baba aliwaambia kwamba alikuwa ameficha kwa siri urithi wao katika sehemu tofauti za bustani. Kila gawio la mtoto lilikuwa na jina lake. Lakini ilikuwa juu yao kutafuta maficho ya siri ambapo gawio lilikuwa limefichwa. Njia pekee ya kufanya hilo ilikuwa ni kulima bustani. Kulikuwa na tahadhari moja tu. Lazima wawe waangalifu ili wasiharibu miti ya matunda!

Hivyo, ulimaji ulianza. Waliilima bustani yote lakini hawakupata hazina yoyote. Wakifahamu baba yao alikuwa mtu mwenye haki ambaye daima alitimiza ahadi zake, waliilima bustani kwa mara ya pili. Wakati huu, walihakikisha wanachimbua vizuri udongo bustanini kote, lakini bado hawakupata hazina yoyote. Sasa, hadi kufikia wakati walipomaliza kulima ardhi kwenye eneo kubwa kwa mara nyingine, waligundua kwamba matawi ya miti ya bustani yalianza kustawi kwa matunda mengi, yaliyoiva. Hivyo waliahirisha ulimaji wao na kila mmoja wao alianza kuchuma matunda ya bustani kulingana na uwezo wake na kuyauza. Hapo ndipo kitendawili cha urithi wa baba yao kilipoteguliwa kwao. Hazina iliyofichwa ilikuwa katika kulima na kuitunza bustani ili izae matunda mazuri. Miti ingeendelea kuzaa matunda mengi mazuri kadiri ambavyo ingetunzwa vizuri. Kwenye kifo chake, baba yao alikuwa amewafundisha kanuni muhimu kwamba pesa inachipua juu ya miti ikiwa wangefanya kazi kwa bidii ya kuitunza miti hiyo. Tangu hapo na kuendelea, waliweka msimamo wa kufanya kazi kwa bidii na kujihifadhia urithi ambao baba yao alikuwa amewaachia.

Fumbo la urithi uliofichwa ardhini ni mfano mzuri wa kazi ya umisionari. Kama mmisionari mtarajiwa kijana, pengine umetumia miaka yako mingi kama kijana ukiwa shuleni na kwa muda huo mwingi ulikuwa chini ya uangalizi wa wazazi wako au walezi. Ikiwa wao ni waumini wa Kanisa, yawezekana walikutambulisha kwenye injili na pengine ushuhuda wako umeimarishwa kwa ushuhuda wao. Tabia zako mwenyewe za kuabudu yawezekana zinafuata tabia walizozianzisha nyumbani—za sala ya familia, usomaji au kujifunza maandiko kifamilia, jioni ya familia nyumbani, kuhudhuria kanisani na kuhudhuria hekalu ikiwa liko karibu. Walilipia ada yako, walikununulia sare za shule na nguo zingine na waligharamia gharama zingine zozote zilizohitajika shuleni pamoja na mahitaji mengine binafsi. Shuleni, maisha yalipangiliwa kwa ajili yako—ratiba ya madarasa na shughuli ilitolewa kwako na uliitimiza vyema. Hukuwa na haja ya wewe binafsi kuwa na wasiwasi kuhusu mambo haya. Hivyo ni kawaida kutarajia kwamba maisha yataendelea kuwa hivyo.

Hata hivyo, kama vile watoto wa mtu tajiri walivyogundua, muda unafika wakati ambapo lazima utegemee ushuhuda wako mwenyewe wa kweli za maisha. Hii huja tu kwa kufanya juhudi binafsi. Ikiwa hutafanya hivyo, yawezekana ukaendelea kuamini kwamba masuluhisho kwenye matatizo ya kawaida ya maisha yako kama mtu mzima yanapaswa kutolewa na wengine. Unaweza kushindwa kutambua jukumu lako mwenyewe katika kutatua magumu ya maisha ambayo bila shaka utakutana nayo kama mtu mzima. Katika mtazamo huo, unaweza kuwa katika hatia ya kuwalaumu wengine kwa kutokukufanyia mambo ambayo unapaswa kuyafanya wewe mwenyewe. Wakati walipoweka juhudi katika kulima bustani, kazi ambayo mwanzo waliiona kama ngumu na isiyo na mvuto, watoto wa tajiri walijifunza kwamba ni juhudi zao wenyewe ambazo zilifichua hazina halisi iliyofichwa ardhini—matunda ambayo yalichanua kadiri walivyolima na kufanya virutubisho vya udongo vipatikane kwenye mizizi.

Kutokana na fumbo hili, ninapendekeza hatua tatu zifuatazo ambazo zitakusaidia kujiandaa vyema kutumikia misheni—uchaguzi ambao utabariki maisha yako milele.

  1. Hatua ya kwanza inaanza kwa kuwa na imani isiyoyumba katika mpango wa Baba wa furaha, uliowezeshwa kwa Upatanisho wa Mwana Wake wa Pekee, Mwokozi wetu Yesu Kristo. Wao wanataka wewe uwe na furaha na ufanikiwe. Wametoa rasilimali na fursa kwa ajili yako kufikia lengo hili wewe mwenyewe. Kutumikia misheni ni mojawapo ya fursa hizo. kuna shangwe kubwa katika kujifunza zaidi na kushiriki mpango wa furaha pamoja na wengine.

Kama vile Alma alivyofundisha, ni muhimu “kuamka na kuziwasha akili zenu, hata kwenye kujaribu juu ya maneno yangu na kutumia sehemu ya imani”1 kwa Wale wanaotafuta furaha yako ya milele na kwa watoto wote wa Baba wa Mbinguni.

  1. Hili litakuongoza kwenye hatua ya pili ambayo ni kutamani baraka hii kwa ajili yako na kwa ajili ya wengine.Utaruhusu “hamu hii ifanye kazi ndani yako, hata mpaka uamini kwa njia ambayo utatoa nafasi kwa sehemu ya maneno yangu”2 kwa imani yako kuwa hai ndani yako. Ikiwa bado hutumikii misheni, kama vile watoto wa mtu tajiri ambao waliamini katika ahadi ya baba yao, utaanza kwa ari kutafuta fursa za kuanza kujiandaa kwa bidii kuhudumu misheni. Utajiunga na darasa la maandalizi ya umisionari ambapo utapata nakala binafsi ya kijitabu cha mafunzo: Masomo ya Maandalizi ya Umisionari, Eneo la Kati la Afrika, kinachopatikana kupitia rais wa akidi yako ya wazee au askofu. Masomo katika kijitabu hiki yamesanifiwa kukusaidia wewe kujaribu kila kanuni unayojifunza ili uweze kupata ushuhuda binafsi wa kweli na nguvu za kanuni hiyo. Kila moja ya masomo kumi na mawili linakualika na kukupa nyenzo za kukuongoza kwenye 1) kutafakari, 2) kujifunza na kujadili, na 3) kujiandaa kupata ushuhuda wako mwenyewe wa kila kanuni katika muda wa wiki kumi na mbili ukikamilisha somo moja kila wiki. Ikiwa tayari unatumikia misheni, utatafuta kupata kijitabu hiki kutoka kwa rais wako wa misheni na kukitumia kufanya upya uelewa wako wa kila kanuni wakati wa kujifunza kwako binafsi na katika kazi yako kila siku.

  2. Kufanya kazi kwa bidii kupitia masomo ya maandalizi ya umisionari ni kama watoto wa tajiri kulima shamba kwa mara ya kwanza. Walimwamini baba yao lakini ulimaji wao wa kwanza haukuleta hazina waliyoitumainia, ingawa yawezekana waliona katika hatua ile kwamba miti ya bustani ilianza kubadilika kwa uzuri. Hatua ya tatu basi ni kufanya kile watoto wa tajiri walichofanya baada ya ulimaji wa kwanza—kuwa makini na mwenye bidii katika kutumia kanuni ulizojifunza wakati unapofika kwenye eneo la misheni kama mmisionari.

Ikiwa utafanya hili, ushuhuda wako wa ahadi ya mpango wa furaha wa Baba kisha utasitawi na misheni yako itakuwa kwako “mti unaochipua kuelekea maisha ya milele”3. Utakuwa chombo katika mikono ya Baba wa Mbinguni kubariki maisha yako mwenyewe, maisha ya wale utakaowatumikia kama mmisionari na familia yako ya baadaye. Unapofanyia kazi kanuni hizi kote katika maisha yako ya baadaye, kutakuwa na nyakati nyingi ambapo mara kwa mara utapokea ushuhuda huu katika moyo wako:“vyema, mtumwa mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu kwenye vichahce, nitakufanya mtawala juu ya vingi: ingia katika shangwe ya Bwana wako”4.

Joseph W. Sitati aliidhinishwa kama Sabini Mkuu mwenye Mamlaka mnamo Aprili 2009. Amemuona Gladys Nangoni; wao ni wazazi wa watoto watano.