2022
Kujiandaa kwa ajili ya Misheni
Machi 2022


UJUMBE WA KIONGOZI WA ENEO HUSIKA

Kujiandaa kwa ajili ya Misheni

Nilitembea maili 224 ili kufika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo—nchi ambayo niliitwa kutumikia misheni yangu.

Kufuatia ubatizo wangu mnamo 20 Agosti 1994, katika Tawi la Makélékélé, Wilaya ya Brazzaville, nilijiuliza mwenyewe swali hili:

Je, ni jinsi gani ninapaswa kujiandaa mwenyewe?

Katika Mafundisho na Maagano 11:21 tunasoma: “Usitafute kulitangaza neno langu, bali kwanza tafuta kulipata neno langu, na kisha ulimi wako utalegezwa; halafu, kama unataka, utapata Roho wangu na neno langu, ndiyo, nguvu ya Mungu kwa kuwashawishi wanadamu.”

Hili lilinisukuma mimi kujiandikisha katika Chuo cha Injili, ambapo nilipaswa kujifunza Kitabu cha Mormoni. Hili liliangaza maisha yangu, likaniruhusu kupata ushuhuda wa injili iliyorejeshwa, Kuja kwa Kristo na kunitia moyo wa kufanya uamuzi wa kutumikia misheni. Nikiwa nimeguswa na utii ulioonyeshwa na Nefi, niliamua kufanya kama alivyofanya katika 1 Nefi 3:7: “Nitaenda na kutenda vitu ambavyo Bwana ameamuru, kwani ninajua kwamba Bwana hatoi amri kwa watoto wa watu, isipokua awatayarishie njia ya kutimiza kitu ambacho amewaamuru.”

Nilipokea wito wangu wa kutumikia misheni wiki moja kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilianza mnamo 18 Desemba 1998, huko Congo Brazzaville, nchi yangu nilipozaliwa. Nilikuwa na miaka 28. Ilinibidi nijibu wito wa Bwana ambao ulitolewa kwangu kupitia mtumishi Wake, Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008). Nilitembea maili 224 ili kufika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo—nchi ambayo niliitwa kutumikia misheni yangu.

Tunapowatumikia ndugu zetu, changamoto huweza kugeuzwa kuwa fursa za kukua. Niliposoma Kitabu cha Mormoni na kutafakari juu ya maandiko, nilikuja kugundua kwamba Bwana alimsaidia Nefi wakati wote. Hilo lilinipa tumaini kwamba Bwana atanisaidi mimi pia kama ningefanya maamuzi sahihi ya kumtumikia Yeye kupitia misheni. Katika uzoefu huu, licha ya vikwazo, nilisonga mbele kwa uhuru, nikiwa na barua yangu ya wito wa misheni kutoka kwa Rais Gordon B. Hinckley, nabii wetu kwa kipindi hicho. Nilihisi uwepo wa Roho wa Bwana katika safari yangu yote ya misheni.

Ni muhimu kujua kwamba mmisionari ni chombo katika mikono ya Bwana na kwamba lengo la mmisionari ni “kuwaalika wengine waje kwa Kristo, kwa kuwasaidia wao wapokee injili iliyorejeshwa kupitia imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, toba, ubatizo, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuvumilia hadi mwisho.”1 Tutapaswaa kutafakari maswali yafuatayo: “Tunaweza kufanya nini ili kujiandaa wenyewe kama tunatamani kufikia lengo hili?

Sisi sote—wazazi, vijana na watoto—tunaweza na tunapaswa kujiandaa kutumikia kama wamisionari—iwe tunatumikia kama wamisionari wa kata au tawi, iwe tunapanga kutumikia katika umri wa ujana au tukitumainia kuitwa hapo baadaye maishani kama wamisionari wazee. Wavulana wanaostahili wanapaswa—na wasichana wanaweza—kuzingatia kutumkia misheni. Zungumza na askofu wako au rais wa tawi. Anaweza kukuongoza kwenye mchakato wa maandalizi kwa ajili ya misheni na kuelewa jukumu la mzazi katika kazi hii.

Katika Mathayo 28:19–20 Bwana amesema: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

Fungu hili linatueleza kwamba ni jukumu la wote wanaomfuata Yeye kujihusisha na kazi ya umisionari. Katika Mafundisho na Maagano 88:81, Bwana alirudia tangazo hili mwanzoni mwa kipindi hiki cha mwisho: “Ni wajibu wa kila mtu ambaye ameonywa amwonye jirani yake.”

Dada Epiphanie Christel Mabiala alizaliwa huko Pointe Noire, Jamhuri ya Kongo. Yeye na mume wake ni wazazi wa watoto watatu. Aliitwa kama Mshauri wa Taasisi wa Eneo mnamo Julai 2021.

Muhtasari

  1. Preach My Gospel: A Guide to Missionary Service [2004], 1.