2022
Ukweli ni nini?—Dondoo
Novemba 2022


Ukweli ni Nini?

Dondoo

Picha
Nukuu ya Nelson kwenye bango

Pakua PDF

Tokea mkutano wetu wa mwisho wa Aprili, tumeshuhudia matukio mengi ya ulimwengu, kuanzia ya kuhuzunisha hadi ya kustaajabisha.

Tunafurahishwa na ripoti za mikutano mikubwa ya vijana inayofanyika kote ulimwenguni. …

Tunashangilia kwamba mahekalu zaidi yanajengwa kote ulimwenguni. …

Unyanyasaji unajumuisha ushawishi wa yule adui. Ni dhambi kubwa. …

Adui anazo mbinu nyingine za kusumbua. Miongoni mwa hizo ni jitihada zake za kuweka ukungu kati ya ukweli na kile kisicho kweli. Mafuriko ya taarifa yanayopatikana kwenye ncha za vidole vyetu, cha kushangaza, inafanya kuwa vigumu zaidi kuamua kile kilicho kweli. …

… Baadhi wangetaka tuamini kwamba ukweli ni kadiri—ambavyo kila mtu anapaswa kujiamulia mwenyewe kile kilicho kweli. Imani kama hiyo ni matamanio tu kwa wale wanaodhani kimakosa kuwa hawatawajibika kwa Mungu.

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, Mungu ni chanzo cha ukweli wote. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linakumbatia ukweli wote ambao Mungu anaufikisha kwa watoto Wake, iwe wamejifunza kutoka katika maabara za kisayansi au umepokelewa moja moja kwa ufunuo kutoka Kwake.

Kutoka kwenye mimbari hii leo na kesho mtaendelea kuusikia ukweli. Tafadhali andikeni mihutasari ya mawazo yanayokuvutieni na yale yanayokuja akilini mwenu na kukaa moyoni mwenu. Kwa sala mwombe Bwana athibitishe kwamba kile ulichokisikia ni cha kweli.