2022
Taji la Maua Badala ya Majivu: Njia ya Uponyaji ya Msamaha—Dondoo
Novemba 2022


“Taji la Maua Badala ya Majivu: Njia ya Uponyaji ya Msamaha—Dondoo,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Taji la Maua Badala ya Majivu: Njia ya Uponyaji ya Msamaha

Dondoo

Picha
Kristin M. Yee
Picha
Nukuu ya Yee kwenye bango

Pakua PDF

Na Nilipokea, na Kristin Yee

Hatuachiwi kushughulika na matokeo ya matendo ya watu wengine peke yetu, sisi pia tunaweza kufanywa wazima na kupewa nafasi ya kuokolewa kutokana na hasira na chuki na matendo yoyote ambayo yanafuata.

… Bwana anatutaka sisi kusamehe kwa faida yetu wenyewe. Lakini Yeye hatuombi sisi tufanye hivyo pasipo msaada Wake, upendo Wake na uelewa Wake. Kupitia maagano yetu na Bwana, tunaweza kila mmoja kupokea nguvu ya kuimarisha, mwongozo na msaada tunaohitaji ili kusamehe na kusamehewa. …

… Yeye alisema “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria masikini habari njema, amenituma kuponya waliovunjika moyo, kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru wale walioteswa” [Luka 4:18; msisitizo umeongezwa].

Kwa wote walivunjika moyo, wafungwa, walioteswa na pengine waliopofushwa na maumivu au dhambi, Yeye anatoa uponyaji, ahueni na ukombozi. Ninashuhudia kwamba uponyaji na ahueni atoayo ni halisi. …

Yesu Kristo ni Masiya wako binafsi, Mkombozi na Mwokozi wako mwenye upendo, anayejua kusihi kwa moyo wako. Anatamani uponyaji na furaha yako. Yeye anakupenda. Analia pamoja na wewe katika huzuni zako na anafurahia kukufanya wewe uwe mzima. Na tujipe moyo na kuushika mkono Wake wenye upendo ambao umenyoshwa wakati tunapotembea njia ya uponyaji ya msamaha.