2022
Jivike Nguvu Zako, Ee Sayuni—Dondoo
Novemba 2022


“Jivike Nguvu Zako, Ee Sayuni—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Jivike Nguvu Zako, Ee Sayuni

Dondoo

Picha
Nukuu ya Bednar kwenye bango

Pakua PDF

Naomba kwa dhati kwamba Roho Mtakatifu atamuangazia kila mmoja wetu wakati tunapozingatia umuhimu wa fumbo la karamu ya harusi ya kifalme. …

Mfalme alipoingia katika ukumbi wa harusi, akautazama umati na mara moja akamwona mgeni mmoja aliyeonekana wazi kutokuwa kwenye vazi la harusi. Mtu yule akaletwa mbele, na mfalme akauliza, “Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la harusi? Naye hakuwa na cha kusema” [Mathayo 22:12]. …

… Mtu yule kukataa kuvaa vazi la harusi kulionyesha utovu wa nidhamu kwa wote mfalme na mwanawe. Hakukosa vazi la harusi; bali, alichagua kutolivaa. … Maamuzi ya mfalme yalikuwa ya upesi na wazi: “Mfungeni mikono na miguu, na mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” [Mathayo 22:13].

… Kutokuwa na vazi linalofaa kulionyesha uasi wake wa ndani dhidi ya mfalme na maelekezo yake.

Fumbo kisha linahitimisha na andiko hili lenye kugusa hisia: “Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache” [Mathayo 22:14].

…Mungu hana orodha ya watu pendwa ambayo sharti tuitazamie kwamba majina yetu siku moja yataongezwa. Hana ukomo kwenye “wateule” kuwa wachache pekee. Badala yake, mioyo yetu, hamu zetu, kuheshimu kwetu maagano na ibada zetu takatifu za injili, utiifu wetu wa amri, na, muhimu sana, neema na rehema ya ukombozi ya Mwokozi huamua kama tunahesabiwa kama mmoja wa wateule wa Mungu. …

Tutafutapo ipasavyo kipawa cha kiroho cha macho ya kuona na masikio ya kusikia, ninaahidi kwamba tutabarikiwa kwa uwezo na uamuzi wa kuimarisha muunganiko wetu wa kimaagano na Bwana aliye hai. Pia tutapokea nguvu za uungu maishani mwetu—na hatimaye tuitwe na kuteuliwa kwa ajili ya karamu ya Bwana.