2022
Mafundisho ya Kuwa Sehemu Ya—Dondoo
Novemba 2022


“Mafundisho ya Kuwa Sehemu Ya—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Mafundisho ya Kuwa Sehemu Ya

Dondoo

Picha
Nukuu ya Christofferson kwenye bango

Pakua PDF

Ningependa kuzungumzia kuhusu kile ninachokiita mafundisho ya kuwa sehemu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

… Hatuwezi kuruhusu ubaguzi wowote, chuki za kikabila au migawanyiko mingine kuwepo katika Kanisa la siku za mwisho la Yesu Kristo. …

Hisia za kuwa sehemu ya ni muhimu kwa ustawi wetu wa kimwili, kiakili na kiroho. Bado, yawezekana kabisa kwamba nyakati zingine kila mmoja wetu anaweza akahisi kutokuwa sehemu ya. …

Na tuache hukumu mikononi mwa Bwana na wale aliowapa mamlaka na sisi tuwe radhi kupendana na kutendeana mema kadiri tuwezavyo. …

Upande wa pili wa mafundisho ya kuwa sehemu ya unahusiana na michango yetu wenyewe. Ingawa mara chache tunafikiria kuhusu hili, sehemu kubwa ya sisi kuwa sehemu ya, hutokana na huduma yetu na dhabihu tunazofanya kwa ajili ya wengine na kwa ajili ya Bwana. …

Kitu cha mwisho na cha muhimu zaidi cha mafundisho ya kuwa sehemu ya ni nafasi muhimu ya Yesu Kristo. Hatujiungi na Kanisa kwa ajili ya ushirika peke yake, japo hilo ni muhimu. Tunajiunga kwa ajili ya ukombozi kupitia upendo na rehema ya Yesu Kristo. Tunajiunga ili kupata ibada za wokovu na kuinuliwa kwa ajili yetu wenyewe na wale tuwapendao kwenye pande zote mbili za pazia. Tunajiunga ili kushiriki katika mradi mkubwa wa ujenzi wa Sayuni kwa matayarisho ya kurudi kwa Bwana.