2022
leo hii—Dondoo
Novemba 2022


“Siku Hii—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Leo Hii

Dondoo

Picha
Nukuu ya Rasband kwenye bango

Pakua PDF

Nimeshikilia nakala ya Kitabu cha Mormoni. Hii ni nakala ya kale ya mwaka 1970 na ni ya thamani kwangu. Kwa mwonekano wake kimechakaa na kuchanika, lakini hakuna kitabu kingine cha muhimu katika maisha yangu na ushuhuda wangu kama hiki. Kwa kukisoma, nilipata ushahidi kupitia Roho kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, kwamba Yeye ni Mwokozi wangu, kwamba maandiko haya ni maneno ya Mungu, na kwamba injili imerejeshwa. …

“Leo hii,” moja ya wamisonari wakuu wa Kitabu cha Mormoni ni Rais Russell M. Nelson. …

… Ametoa nakala za Kitabu cha Mormoni kwa mamia ya watu, mara zote akitoa ushuhuda wake wa Yesu kristo. …

Nabii wetu aishiye anafanya sehemu yake kwenye kuijaza dunia kwa Kitabu cha Mormoni. Lakini hawezi kufungua milango peke yake. Yatupasa kufuata mfano wake. …

… Ninawaalika, leo hii, kuwapa marafiki na familia zenu Kitabu cha Mormoni, wafanyakazi wenzenu, kocha wa timu yenu ya mpira wa miguu, au mzalishaji sokoni kwenu. Wanahitaji maneno ya Bwana yapatikanayo kwenye kitabu hiki.

Ninashuhudia kwamba kwa mpango matakatifu Kitabu cha Mormoni kiliandaliwa huko Amerika ya kale ili kuja kutangaza neno la Mungu, kuleta nafsi kwa Bwana Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho “leo hii.”