2022
Aliinuliwa Juu ya Msalaba—Dondoo
Novemba 2022


“Aliinuliwa juu ya Msalaba—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Aliinuliwa Juu ya Msalaba

Dondoo

Picha
Nukuu ya Holland kwenye bango

Pakua PDF

Sababu moja ya kwa nini hatutilii mkazo msalaba kama alama inatokana na vyanzo vyetu vya Kibiblia. Kwa sababu kusulubiwa ilikuwa moja ya njia kali sana za kuua za utawala wa Kirumi, wafuasi wengi wa mwanzoni wa Yesu walichagua kutoangazia aina hiyo ya kikatili ya mateso. Maana iletwayo na kifo cha Kristo kwa hakika ilikuwa kitovu cha imani yao, lakini kwa takribani miaka 300 walitafuta kufikisha utambulisho wao wa injili kupitia njia zingine. …

Sababu nyingine ya kutotumia alama ya msalaba iliyopo ni msisitizo wetu juu ya muujiza kamili wa huduma ya Kristo—Ufufuko Wake mtukufu pamoja na mateso na kifo chake cha kidhabihu. …

…Katika kila nchi na umri, Yeye amesema kwetu sote, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate” [Mathayo 16:24].

Hii inaongelea juu ya misalaba tunayoibeba kuliko ile tunayoivaa. Kuwa mfuasi wa Yesu Kristo, mtu lazima wakati mwingine abebe mzigo—wa kwako mwenyewe au wa mtu mwingine—na kwenda mahali ambako dhabihu inahitajika na mateso hayaepukiki. Mkristo wa kweli hawezi kumfuata Bwana kwa masuala yale tu ambayo yeye anakubaliana nayo. La hasha. Tunamfuata Yeye kila mahali, ikijumuisha, kama ni muhimu, ndani ya viwanja vilivyojaa machozi na taabu, ambapo wakati mwingine yawezekana tukasimama peke yetu.

… Naomba tumfuate Yeye—bila kushindwa, pasipo kuyumba wala kukimbia, pasipo kutegea katika jukumu, siyo tu wakati misalaba yetu ni mizito na siyo wakati, njia inapozidi kuwa na kiza.