2022
Yesu Kristo Ni Nguvu kwa Vijana—Dondoo
Novemba 2022


“Yesu Kristo ni Nguvu kwa Vijana—Dondoo,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Yesu Kristo Ni Nguvu kwa Vijana

Dondoo

Picha
nukuu ya kwenye bango

Pakua PDF

Kama upo kati ya umri wa miaka 11 na 18, nina ujumbe mahususi kwako kutoka kwa Mwokozi, Yesu Kristo.

Ujumbe wa Mwokozi Kwako

Rafiki zangu vijana wapendwa, kama Mwokozi angekuwepo hapa sasa hivi, Je, Yeye angesema nini kwenu?

Ninaamini angeanza kwa kuonyesha upendo Wake wa dhati kwenu.

Lakini bado, kwa sababu sote tu wadhaifu na tusio kamili, baadhi ya dukuduku zingekuja mawazoni mwenu. Mngeweza kukumbuka makosa mliyoyafanya, nyakati ambazo mlishindwa na jaribu, vitu ambavyo mngetamani msingevifanya—au ambavyo mngevifanya vizuri. …

Ninaamini Mwokozi Yesu Kristo angewataka muone, kuhisi na kujua kwamba Yeye ni nguvu yenu. Kwamba kwa msaada Wake, hakuna mwisho wa kile mnachoweza kutimiza.

Mwokozi angetamka, kwa virai dhahiri, kwamba wewe ni binti au mwana wa Mungu Mwenyezi. Baba yako wa Mbinguni ni mtukufu zaidi ya wote katika ulimwengu, mwingi wa upendo, furaha, usafi, utakatifu, nuru, rehema na ukweli. Na siku moja Anataka ninyi mrithi vyote Alivyonavyo. …

Ili kuwezesha hili, Alimtuma Yesu Kristo kuwa Mwokozi wenu. …

Hiyo ndiyo takdiri yenu. Hiyo ndiyo kesho yenu. Huo ndiyo uchaguzi wenu!

Ukweli na Chaguzi

Kiini cha mpango wa Mungu kwa ajili ya furaha yenu ni nguvu yenu ya kufanya chaguzi. …

Wakati una chaguzi muhimu za kufanya, Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho ni uchaguzi bora zaidi. Unapokuwa na maswali, Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho ni jibu bora zaidi. Unapohisi dhaifu, Yesu Kristo ni nguvu yako. …

Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana

Ili kuwasaidia kuipata Njia na kuwasaidia kufanya mafundisho ya Kristo kuwa mwongozo wenye ushawishi katika maisha yenu, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho limeandaa nyenzo mpya, iliyopitiwa upya ya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana. …

Nikiweka wazi, mwongozi bora kushinda wote mnaoweza kuwa nao katika kufanya chaguzi ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni nguvu kwa vijana.

Hivyo dhumuni la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ni kuwaelekeza Kwake. …

Pia ni muhimu kujua kile Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana haikifanyi. Haifanyi chaguzi kwa ajili yenu. Haiwapi “ndio au “hapana” kuhusu kila uchaguzi ambao mnaweza kukutana nao. Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana inafokasi kwenye msingi kwa ajili ya chaguzi zenu. Inafokasi kwenye maadili, kanuni na mafundisho badala ya kila tabia maalum. …

Je, ni vibaya kuwa na sheria? Hapana. Sote tunazihitaji kila siku. Lakini ni vibaya kufokasi kwenye sheria pekee badala ya kufokasi kwa Mwokozi. …

Kiwango cha Juu

Yesu Kristo ana viwango vya juu sana kwa wafuasi Wake. Na mwaliko wa dhati kutafuta mapenzi Yake na kuishi kulingana na kweli Zake ni kiwango cha juu kinachowezekana!

Maamuzi muhimu ya kimwili na kiroho hayapaswi kuwa tu ni mapendeleo binafsi, au kile ambacho ni kawaida kwetu au maarufu. Bwana hasemi, “Fanya utakavyo.”

Anasema, “Acha Mungu Ashinde.”

Anasema, “Njoo, unifuate.”

Anasema, “Ishi katika njia takatifu, ya juu na ya kukubalika.”

Anasema, “Zishike amri Zangu.”

Yesu Kristo ni mfano wetu mkamilifu, na tunajitahidi kwa nguvu zetu zote kumfuata.

Rafiki zangu wapendwa, acha nirudie, kama Mwokozi angesimama hapa leo, Angeonyesha kwenu upendo Wake usio na mwisho, imani Yake yote kwenu. Angewaambia kuwa mnaweza kufanya hili. Mnaweza kujenga maisha ya shangwe na furaha kwa sababu Yesu Kristo ni nguvu yenu. Mnaweza kupata kujiamini, amani, usalama, furaha, na kuhisi kupendwa sasa na milele, kwa sababu mtapata yote katika Yesu Kristo, injili Yake, na kwenye Kanisa Lake.