2022
Urithi wa Uhimizaji—Dondoo
Novemba 2022


“Urithi wa Uhimizaji—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Urithi wa Uhimizaji

Dondoo

Picha
Nukuu ya Eyring kwenye bango

Pakua PDF

Kama vile mama yangu alivyoniambia nilipolalamika juu ya jinsi jambo lilivyokuwa gumu, “Oh, Hal, bila shaka, ni gumu. Inapaswa kuwa hivyo. Maisha ni mtihani.”

Angesema hivyo kwa upole, hata kwa tabasamu, kwa sababu alijua mambo mawili. Bila kujali pambano, kile kilichokuwa muhimu sana kilikua kufika nyumbani kuwa na Baba yake wa Mbinguni. Na alijua angeweza kufanya hivyo kupitia imani katika Mwokozi wake. …

Urithi wa uhimizaji aliotuachia unaelezwa vyema katika Moroni 7, ambapo Mormoni anawahimiza mwanawe Moroni na watu wake. …

Anamweka Yesu Kristo kwanza, kama wanavyofanya wale wote wafanikiwao katika kutoa uhimizaji kwa wale wapambanao kupanda juu kwenye njia ya kwenda nyumbani kwao mbinguni. …

Mormoni aliona unyenyekevu kama ushahidi wa nguvu za imani yao. …

Mormoni kisha anawahimiza wao kwa kuwashuhudia kuwa walikuwa kwenye njia ya kupokea kipawa cha mioyo yao kujawa na upendo safi wa Kristo. …

Nikitazana nyuma, sasa naona jinsi kipawa cha hisani—upendo msafi wa Kristo—kilivyomuimarisha, kilivyomwongoza, kilivyomhimili na kilivyombadilisha mama yangu katika pambano kwenye njia yake kurudi nyumbani. …

… Mwokozi anajua mapambano yako kwa undani. Yeye anajua uwezekano wako mkubwa wa kukua katika imani, tumaini na hisani.

Amri na maagano anayoyatoa kwako si mitihani ya kukudhibiti. Ni vipawa vya kukuinua kuelekea kupokea vipawa vyote vya Mungu na kurejea nyumbani kwa Baba yako wa Mbinguni na Bwana, ambao wanakupenda.