2022
Kuwa Mkweli kwa Mungu na Kazi Yake— Dondoo
Novemba 2022


“Kuwa Mkweli kwa Mungu na Kazi Yake—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kuwa Mkweli kwa Mungu na Kazi Yake

Uruguay

Picha
Nukuu ya Cook kwenye bango

Pakua PDF

Mojawapo ya mifano yenye msukumo katika maandiko ya … kuhusu kutafuta ushuhuda wa kazi ya Mungu na Yesu Kristo umeelezwa katika ushauri wa Alma kwa wanawe watatu—Helamani, Shibloni, na Koriantoni. …

Wasiwasi wa kwanza wa Alma … ulikuwa kwamba kila mmoja apate kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo na kuwa mkweli kwa Mungu na kazi Yake.

… Shibloni alikuwa mwadilifu, kama kaka yake Helamani. Ushauri ninaotaka kusisitiza ni Alma 38:12, ambao kwa sehemu unasomeka hivi, “Uone kwamba ujifunze kuzuia tamaa zako zote, ili uweze kujazwa na upendo.”

… Mwili si mwovu—ni mzuri na ni muhimu—lakini baadhi ya shauku, zisipotumiwa ipasavyo na kwa udhibiti, zinaweza kututenganisha na Mungu na kazi Yake na kuathiri vibaya ushuhuda wetu. …

Zaidi ya kudhibiti hasira na kudhibiti tamaa nyinginezo, tunahitaji kuishi maisha safi ya kimaadili kwa kudhibiti mawazo, lugha, na matendo yetu. …

Kwa sababu Koriantoni alikuwa amejihusisha na uasherati, ilikuwa muhimu kwa Alma kumfundisha kuhusu toba. …

Kwa hivyo, ushauri wa namna ya kuzuia wa Alma ulikuwa ni kudhibiti tamaa, lakini ushauri wake kwa wale ambao wamevunja sheria ulikuwa kutubu. …

Hakuna awezaye kurudi kwa Mungu kwa juhudi zake pekee, sote tunahitaji msaada wa dhabihu ya Mwokozi. Wote wamefanya dhambi, na ni kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo pekee ndipo tunaweza kupata rehema na kuishi na Mungu.