2023
Ni kwa Jinsi Gani Tunaweza Kuifanya Mikusanyiko Yetu Iwe yenye Umoja Zaidi?
Septemba 2023


Ni kwa Jinsi Gani Tunaweza Kuifanya Mikusanyiko Yetu Iwe yenye Umoja Zaidi? Liahona, Nov. 2023, 44.

Njoo, Unifuate

1 Wakorintho 10–12

Ni kwa Jinsi Gani Tunaweza Kuifanya Mikusanyiko Yetu Iwe yenye Umoja Zaidi?

Picha
Vitendo tofauti ambavyo vinaweza kukuza umoja miongoni mwa waumini wa Kanisa

Kielelezo na Vicky Scott

Paulo alisikia kulikuwa na migawanyiko miongoni mwa waumini wa Kanisa katika mji wa Korintho (ona 1 Wakorintho 11:18). Katika kujibu, yeye aliwasihi katika barua “ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe” (1 Wakorintho 12:25).

Tunaweza kuonesha “viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe” kupitia vitendo visivyo na ubinafsi vya upendo na hisani. Paulo alitaja njia kadhaa tunazoweza kufanya hivyo ili kufanya uhusiano wetu uwe wenye umoja zaidi.

Kufurahia pamoja na kuomboleza na wengine.

“Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho” (1 Wakorintho 12:26).

Fanya matendo yasiyo na ubinafsi ya huduma.

“Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake” (Tafsiri ya Joseph Smith, 1 Wakorintho 10:24 [katika 1 Wakorintho 10:24, tanbihi b]).

Kuunganika katika shuhuda zetu za Mwokozi.

“Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja [wa Kristo]” (1 Wakorintho 10:17).

Mpende kila mtu.

“Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu” (1 Wakorintho 10:32).