2023
Ni kwa Jinsi Gani Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu Hutusaidia Tutubu?
Septemba 2023


“Ni kwa Jinsi Gani Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu Hutusaidia Tutubu?,” Liahona, Sept. 2023.

Njoo, Unifuate

2 Wakorintho 7

Ni kwa Jinsi Gani Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu Hutusaidia Tutubu?

Picha
Yesu akimkumbatia mtu

Picha na Mark Mabry

Mtume Paulo alifunza “ huzuni iliyo kwa jinsi ya mungu huleta toba iletayo wokovu … lakini huzuni ya ulimwengu hufanya mauti” (2 Wakorintho 7:10). Tunaweza kuhisi huzuni ya ulimwengu, aibu, na kuvunjika moyo tunapotenda dhambi. Na bado tunaweza kumgeukia Mwokozi ili tutubu, tunamwalika Yeye kubadilisha mioyo yetu na kuigeuza huzuni yetu kuwa furaha (ona Alma 36:18–20).

Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu na Toba ya Kweli

Tunapohisi huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu, tunatambua mapungufu yetu na kutaka kufanya vyema. Tunahisi tumaini kwa ajili ya siku zijazo—na upendo wa Mwokozi kwa ajili yetu.

Fikiria maswali haya unaposoma 2 Wakorintho 7:

  • Inamaanisha nini kuwa “mlihuzunishwa, hata mkatubu”? (mstari wa 9).

  • Ni hatua zipi tunachukua wakati tunapohisi huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu? (ona mistari 10–11).